black abdu
Senior Member
- Dec 2, 2022
- 156
- 212
Tanzania ni nchi iliyojaaliwa kuwa tofauti na nchi zingine za Afrika Mashariki na Afrika; kijiografia imebarikiwa kuwa na eneo kubwa la ardhi kutosha kwa kilimo, vyanzo vya maji na bahari yenye ukanda mrefu wa pwani na vivutio vya utalii vyenye umaarufu mkubwa duniani. Kijamii, imebahatika kuwa na idadi kubwa ya watu kwa nguvukazi na jamii inayoishi kwa amani na maelewano licha ya tofauti kubwa ya makabila iliyonayo. Kwa upande wa kisiasa, licha ya changamoto kadhaa, imekuwa na sifa ya kipekee Afrika ya kuwa na mtindo wa kupokezana madaraka bila kusababisha hali ya wasiwasi kwa wananchi tofauti na ilivyo kwa nchi nyingi za Afrika.
Hata hivyo licha ya kuwa na zaidi ya sifa hizo hapo juu, hali haijiakisi kwenye kiwango cha maisha ya jamii kwa vile idadi kubwa ya wananchi wanaishi kwenye umasikini wakitegemea kilimo cha kujikimu. Pia huduma duni za kijamii zinazotokana na sera zisizokidhi uhitaji na uzembe wa watumishi, uchumi wa kusuasua na thamani ya shilingi kuporomoka. Hata hivyo uwepo wa kundi la wachache wenye kipato kikubwa dhidi ya wengi wenye kipato duni ni ishara ya kuwepo na mgawanyo usio sawa wa mapato ya nchi. Hali ambayo inaleta swali la kutafakari kwa uongozi uliopo na uhitaji wa kufanya mabadiliko ili kuleta Tanzania mpya.
Kwa Tanzania ninayoitaka nitaweka mpango wa muda mfupi na mpango wa muda mrefu kama ifuatavyo:
Mpango wa muda mfupi utalenga zaidi kwenye kujenga utashi wa watumishi wa sekta ya umma ili kuboresha upatikanaji wa huduma na kupunguza malalamiko na kumaliza tatizo la rushwa. Idara hizi ni pamoja na mahakama, polisi, vituo vya afya, vituo vya elimu (shule na vyuo), kilimo, usafiri wa umma na sekta ya utumishi wa umma ambayo kwa kiasi kikubwa inaongoza kwa kulalamikiwa kwa uduni wa huduma. Yatakayofanyika ili kujenga utashi ni:

- Mafunzo ya maadili ya kazi na kuongeza uelewa wa watoa huduma juu ya huduma wanazozitoa ili kuondosha usumbufu na kutunza muda kwa kutoa huduma sahihi kwa wakati sahihi kwa kila mwanachi bila kubagua wala kupendelea baadhi na kudharau wengine.
- Kuongeza idadi ya watumishi wa ndani wenye uwezo wa kuongoza vitengo nyeti na vya juu kwenye idara nyeti kama vile madini, bandari na nishati ili kupunguza uhitaji wa wataalamu kutoka nje
- Kuboresha teknolojia, vifaa na mifumo ya utoaji huduma kijitdali ili kuendana na kasi ya maendeleo ya dunia. Hii ni kwa idara na vitengo vyote, kunzia ofisi za umma, vituo vya afya, bandari, polisi na mahakama.
- Kutoa elimu zaidi ya uraia ili kujua haki zao na waweze kuzidai popote wanapokwenda kupata huduma bila kukubali kunyanyaswa, kudharauliwa, kupuuzwa wala kucheleweshwa kwa makusudi au kuombwa rushwa.
- Kuboresha wigo wa utoaji maoni ili wawe wazi kuzungumza panapokuwa na uhitaji wa kufanyika maboresho, kutoa fikra zao juu ya mwenendo na mustakabali wa Taifa na kutumia vema uhuru wao katika kufanya chaguzi sahihi bila kuhitaji kununuliwa au kurubuniwa.
- Mpango wa kukuza uchumi kwa maendeleo endelevu; kuunda sera bora za kuboresha utalii na misitu, kuanzisha viawanda vya vito vya kutumia madini tuliyonayo, viwanda vya kusindika nyama na samaki, skimu za umwagiliaji kwa kilimo kipana cha biashara,
- Kuunda mfumo wa matumizi bora wa mapato ya serekali kwa kuelekeza kiasi kikubwa cha bajeti kwenye miradi ya kimaendeleo badala ya kuelekeza kwenye matumizi ya kawaida ya serekali kama ilivyo sasa, ambapo kiasi kikubwa cha bajeti kinaelekezwa kwenye matumizi ya kawaida ya serekali kuliko kwenye miradi ya kimaendeleo. Pia kupunguza gharama za safari na misafara na ununuzi wa magari ya bei kubwa kwa matumizi ya kazi za serekali. Tukiboresha matumizi ya teknojia ya mawasiliano tunaweza kupunguza uhitaji wa kuandaa mikutano mingi ambayo inaweza kufanyika kwa njia ya mtandao.
- Kujenga vyanzo vya uhakika vya nishati hasa kutumia nishati ya atomiki na jua na kuacha maji yatumike zaidi katika kumwagilia mashamba na kunyweshwa mifugo na misitu. Tutapata nishati ya kutosha kuendeshea mitambo viwandani na treni za mwendo wa kasi kwa uhakika zaidi ili kuboresha huduma zetu za usafirishaji. Pia nishati hii itasaidia kuboresha hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida kwa kuachan na matumzi ya kuni na mkaa. Hapo tutakuwa pia tumeokoa misitu yetu kutoka kukatwa ka ajili ya mkaa.
- Kuboresha sera za uwekezaji na kuwezesha wawekezaji wa ndani hasa vijana ili kuongeza idadi ya walipa kodi. Hii itasaidia pia kuongeza idadi ya kundi la vijana wenye ajira na kupunguza idad ya vijana wasio na ajira.
- Fedha zitakazopatikana kwa kukua kwa uchumi zitasaidia kuboresha maisha ya wananchi kwa kuboresha sekta ya elimu, kutoa huduma za afya bure kwa wasiojiweza, wazee na wenye mahitaji maalumu. Kutoa huduma za bure kwa wagonjwa wenye magonjwa yasiyoambukiza na ya muda mrefu kama figo, kisukari, na saratani. Pia itatumika kuboresh makazi ya wazee na wasiojiweza kuwa na makazi wanaoishi mitaani ili kuruhusu watoto wao kusoma.
Upvote
1