Kujengea kwenye simu: Inatia uchungu sana

Kujengea kwenye simu: Inatia uchungu sana

Aisee inaumiza sana
Kuna sehemu napitaga nikiwa naenda kazini wamejenga mabandavyumba vitatu na vyoo aisee kuanzia msingi niliona ni tatizo na kilasiku nikipita nakuta fundi tu pekeyake imeisha Sasa aisee ni huzuni km mwenyew Yuko mbali atakuja kulia
 
Sasa mimi naongea kama engineer hapa mwenye authority.

Na kama huyo jamaa mwenye hiyo nyumba yupo humu JF anisikilize kwa makini sana asije akaingizwa hasara na huyo ‘Charlatan’ wa mtaani anaejifanya fundi mtaalam kumbe utaalam wake ni kutumia smartphone na kutia watu hasara tu, fundi maana yake utafute mbinu mbadala za kutatua tatizo bila kumuumiza mteja, lenyewe na bichwa komwenlake linakimbilia kuvunja tu, jinga kwelli.

Hapo kuna remedial measure za kawaida tu zinaweza kutatua hayo makosa.

1.) Idadi ya kozi za msingi kuwa chache.

- SI KWELI!!! Hizi idadi ya kozi 5 za kiuno (Plinth) siztatizo, na kamwe si kigezo cha kuvunja, bali remedy hapo ni kukwangua hilo tope la juu lenye mfinyanzi na kuliondoa kabisa site, kisha linatandikwa zulia la kuzuia unyevu (Damp proof membrane) , kisha kinawekwa kifusi kingine kigumu na kuwekwa kama tabaka gumu na imara, kifusi kinaachofaa ni kama kila kinachotumika kwenye ujezi wa barabara, (kifusi cha rangi ya ubuyu), hivyo idadi ya kozi za kiuno zinabaki zile zile 5.

2.) Msingi kukosa mkanda zege.

- Tatizo hili si la kuvunja nyumba, maana kuna remedial measures za kulitatua. Hatua ya kwanza ni kuacha ‘Natural settlement itokee, ambapo unaweza ukaacha nyumba ikae hata miezi 6 bila kuijenga, unaicha ititie yenyewe hadi itakapofika kwenye ‘settlement threshold’, ambapo hapo inakuwa haina uwezo wa kutitia tena kwa kiwango kikubwa, ambapo baada ya hapo utitiaji unakuwa ‘negligible’. Baada ya ‘Settlement threshold’ kufikiwa, unasuka ‘lental’ yenye nondo 3 hadi 4, baada ya kumwaga hiyo rinta, unasubiri tena kama mwezi mmoja ili kuona kama bado kuna ‘residual settlement’ itaendelea, na itakuwa vizuri sana kama mvua itapiga ili kudhibitisha kweli hakuna utitiaji wa ziada. Ukivuka hatua hii umewini. Maana crack zote unakuwa umeshazijua, na crack zinazibika vizuri kwa nondo au wire mesh.

3.) Sebule na choo kuwa na size ndogo.

Hili tatizo linarekebishika kwa urahisi bila gharama kubwa. Cha kufanya ili kuongeza ukubwa wa sebule, na kuvunja hako kaukuta kanakotenganisha sebule na choo, hapo sebule inakuwa imeongezeka ukubwa adequately, halafu kulingana na ramani, chockinaweza kuwekwa ‘semidetached’ kikiunganika na chumba kwa nje, problem solved.

4.) Dirisha kuwa na kozi 3
Hili pia hata layman asiyejua chochote atajua kwamba hili si tatizi la kusababisha uvunje nyumba, maana kozi 3 ndio standard, na akama ukihitaji kozi 2 si unabg’oa tu tofali chache za kozi ya 3 kwenye dirisha kisha zinabaki kozi 2, hakuna issue hapa.

Hilo jamaa linalojiita Mr.Decoration haliumizi kichwa kumsaidia mteja, badala yake linataka lionekane litaalama, kumbe bogus tu.

Na kama huyo taahira anayejiita Mr.Decoration ana pingamizi lolote juu ya analysis yangu, afungue akaunti hapa JF aje apinge.
 
Ila watu wengine bhana. Piga hela ila jenga kitu cha kueleweka basi! Yaani hela imetumika kujenga kitu cha ajabu kabisa.
 
Acha wewe kujifanya mtaalam kuliko huyo Bwana wa Youtube 🙂
Jamaa anajitangaza sana lakini kila nikiangalia nyumba zake sioni workmanship ambayo naitegemea kwa fundi anayejigamba vile.
Mimi sio engineer. Bila shaka anajua megi kuhusu ujenzi kuliko mimi.
Lakini kwa macho ya layman sioni ubora wa kazi zake.
Angalia kuta na nguzo za hizi nyumba anazojivunia.
Sio najifanya mtaalam. Nimetoa hoja, hivyo hoja kwa hoja.

Awe amejenga vizuri au vibaya, point yangu ni kwamba kamtia mwenzake hasara kubwa bila sababu za msingi
 
Back
Top Bottom