Kujiajiri bila mtaji inawezekana

Shusha vitu mkuu...
Mtaji unaweza ukawa kitu chochote ambacho kina-facilitate wewe kutoa huduma au bidhaa fulani ambayo mwisho wa siku itakunufaisha katika kupata unachotaka....

Wewe ukiwa mshona viatu (mtaji ni ujuzi wako) wewe ukiwa mwaminifu (mtaji ni uaminifu wako unaweza ukapewa mali kauli ili uuze); wewe ukiwa una ujuzi fulani ukaajiriwa na kulipwa pesa (mtaji ni ujuzi wako) wewe ukiamka asubuhi na kuweka bundle kwenye simu na kufanya vijikazi ambavyo vinalipa peanuts (hapo zaidi ya mtaji wa bundle ingawa unaweza kwenda sehemu kuna wi-fi bure) mtaji hapo utakuwa muda wako (sababu huo muda huenda wengine wanatumia kufanya mambo makubwa zaidi)

Wewe ukiwa unakubaliwa na vimama vizee vizee kutona na muonekano wako na wanapenda company yako na ukawa escort unawasindikiza sehemu au ukawa GIGOLO, mtaji ni muonekano wako...
 
Sawasawa nimekuelewa vyema mkuu..
Sasa mtu tayari ana bando na vitendea kazi vingine wewe kama wewe unamsaidiaje maaana maneno yamekua mengi huku mitandaoni wakati uhalisia haupo hivo mtaani..
 
Sawasawa nimekuelewa vyema mkuu..
Sasa mtu tayari ana bando na vitendea kazi vingine wewe kama wewe unamsaidiaje maaana maneno yamekua mengi huku mitandaoni wakati uhalisia haupo hivo mtaani..
Hakuna kazi rahisi; Hivyo vikazi mitandaoni kama wengi wanafanya basi demand huenda ni kubwa kuliko supply kwahio kupelekea mtu kulipwa ujira mdogo kulinganisha na mtaji wake wa muda....

Ili ufanikiwe online zaidi ya affiliates na mambo kama hayo unahitaji content na content hiyo lazima iwe na walaji (community) na hio community ili uwalishe kitu bila competition ni vema kwenda kwenye Niche Market (hayo yote yanahitaji mtaji wa muda) Kama wewe unajua kupiga story unaweza ukaanzisha community Youtube mkapiga umbea kwa miaka kadhaa ujishatengeneza watu wengi wakakuelewa unaweza kuanza kutangazia magazeti na vitabu vya umbea ili watu wako wanunue (na wewe hapo unakula commission)

Kwahio inahitaji ku-build community; leo wewe hata ukianzisha JF kama JF yako hata ikiwa nzuri kama JF itakuchukua miaka mingi kwa watu kukuelewa na kama JF ipo kwanini waje kwako ? Ndio hapo labda utafute Niche Market - Kwamba JF yako wewe ni tofauti watu wakitoa Likes sio Likes pekee bali unapewa pesa (share of profit from matangazo) Ingawa JF akiona wewe unafanya hivyo na tayari ana watu na uwezo kuliko wewe anaweza kufanya unachofanya hence uka-fail even before starting....

In short umiza kichwa na tumia muda ku-build community hakuna shortcut ingekuwa rahisi kwanini mimi nisifanye nikwambie wewe ? (lakini huenda wewe ni interest yako ambayo mimi sina na kama that is the case basi fanya - sababu kama ni hobbie who cares hata kama hakuna malipo)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…