Halima na wenzake hawahamii CCM kwa kwa vile bado hawajafukuzwa CDM. Wamezuiliwa kuwa viongozi, bado wanachama. Azimio sio uamuzi. Wataendelea kuwa wabunge na azimio halitapitishwa!
Wajinga ndio waliwao. Waume zao, wajumbe wa kamati kuu si wajinga na ndio maana wamevuliwa nyadhfa zote lakini cc imeazimia kuwafukuza uanachama.
Kwa nini wasingewafukuza uanachama tu halafu nyadhfa zingeondoka automatically?
Wameanza kuwavua nyadhfa, wakafuata kuweka azimio la kuwafukuza uanachama. Kwa nini maneno yooote haya, kwa nini sarakasi zote hizi?
Wale ni wabunge, na mpaka chama kipeleke taarifa kwa spika ya kuwafuta wanachama wake uanachama hapo ndipo Mbunge anavuliwa ubunge wake na si kwa azimio tu tena kwa matangazo ya youtube