Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Licha ya umuhimu wa kuboresha maarifa kazini bado suala hili limekuwa na ukakasi mwingi kuliko mianya bora ya ufanisi. Licha ya wawakilishi wa mwajiri kuwatatavwatumishi wengi kujiendeleza kwa gharama zao wenyewe kimasomo bado sheria ya kutumikia muda wa daraja la mshahara ni changamoto kwa watumishi wanaojiendeleza.
Hakuna njia nyepesi wala njia rahisi kwani kusoma kwa njia ya masafa marefu ni changamoto na kukaa darasani nako kunaambatan na sheria nyingi zinazombana mtumishi anayejiendeleza. Mathalani kuhudhuria kazini wakati wote wa likizo endapo mwajiri atakuhitaji.
Serikali yetu kama ina nia njema na ubora, tija na na maendeleo endelevu yanayosaidia kuboresa utendaji ni vyema ikiliangalia suala hili kwa makini zaidi.