Kujiita Mesi au Tshabalala ni haki au ni ushamba?

eddy brown

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
414
Reaction score
314
Napata shida kuelewa kwa nini mchezaji ajiite jina la mchezaji mwingine.Kwa nini na wewe usitengeneze jina lako kama unajiami.Mfano Muhamed Hussein aka Tshabalala akiuzwa South bado atajiita hivyo wakati mwenye jina yuko pale.Kibadeni alisema anawashangaa wanao fanya hivyo kwani enzi zao walijitengenezea majina yao kama yeye King Kibaden,Sundey Manara Computer.Na nyi wa sasa tengenezeni ya kwenu sio kukopi ya wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini unajiita Eddy Brown wakati wewe ni mswahili na una jina la kienyeji?
 

Na vipi kujiita, Cannavaro?
 
Mimi ndo hapo ninaposhindwa kuelewa hata watu nninao amini wanaujua na kuuishi Mpira wanapouelezea tofauti.

Mfano utamsikia gwiji wa Mpira wa bongo anasema tatizo la mashabiki wa kibongo wanashangilia magoli tu, wakati Ulaya wanashangilia muda wote, nimejaribu kulifuatilia hili.

Nilichokiona ni sawa tu nayale ninayoyaona Taifa mashabiki sehemu kubwa wanashangilia Matukio, goli,chenga,kanzu, pasi mfululizo na Ufundi wa soka.

Isipokuwa kuna vikundi mbalimbali ambayo kazi yake ni ushangiliaji Mwanzo, kati na mwisho wa mchezo.

Timu ambayo imetawala Mpira na imefunga goli hao mashabiki wake watakuwa na furaha muda wote ila wale waliofungwa na kutawaliwa watakuwa Kimyaaaa huku wakiibuka Mara moja moja kwa matukio hili lipo dunia nzima ya mashabiki.

Narudi kwenye hoja Majina ya wachezaji waliowengi hawajipachiki wao wenyewe majina haya hupewa na mashabiki wao au watangazaji wa soka.

King na Computer ni majina waliopewa na mashabiki wao enzi hizoo wakiwa wachezaji nguli, EZEKIEL GREYSON "JUJUMEN" huyu alipachikwa jina hili na mtangazaji AHMED JONGO enzi hizo.

MAHMOUD ABBAS Kenya one huyu alipachikwa jina hili na watangazaji wa soka wa kenya ,huku watangazaji wa Tanzania wakiiga IGA kwa makipa wetu.
 
Wanachosha sana. Utasikia john boko adebayor
 

Kwani anajiita au watu wanamwita!
 
Hivi wanajiita wenyewe au mashabiki wao ndio wanawabandika hayo majina?

"A voice of one calling in the wildernes"
 
Kwanini unajiita Eddy Brown wakati wewe ni mswahili na una jina la kienyeji?
usiseme kienyeji hilo ni tusi/kujidharau. wewe sema tu jina lako la likiswahili/kibantu/kiafrika.yaan kwanini usione fahari kuitwa jina la nyumbani mf mkude,masawe,nyahonyo,wambura,butiku,njoroge nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…