Mimi ndo hapo ninaposhindwa kuelewa hata watu nninao amini wanaujua na kuuishi Mpira wanapouelezea tofauti.
Mfano utamsikia gwiji wa Mpira wa bongo anasema tatizo la mashabiki wa kibongo wanashangilia magoli tu, wakati Ulaya wanashangilia muda wote, nimejaribu kulifuatilia hili.
Nilichokiona ni sawa tu nayale ninayoyaona Taifa mashabiki sehemu kubwa wanashangilia Matukio, goli,chenga,kanzu, pasi mfululizo na Ufundi wa soka.
Isipokuwa kuna vikundi mbalimbali ambayo kazi yake ni ushangiliaji Mwanzo, kati na mwisho wa mchezo.
Timu ambayo imetawala Mpira na imefunga goli hao mashabiki wake watakuwa na furaha muda wote ila wale waliofungwa na kutawaliwa watakuwa Kimyaaaa huku wakiibuka Mara moja moja kwa matukio hili lipo dunia nzima ya mashabiki.
Narudi kwenye hoja Majina ya wachezaji waliowengi hawajipachiki wao wenyewe majina haya hupewa na mashabiki wao au watangazaji wa soka.
King na Computer ni majina waliopewa na mashabiki wao enzi hizoo wakiwa wachezaji nguli, EZEKIEL GREYSON "JUJUMEN" huyu alipachikwa jina hili na mtangazaji AHMED JONGO enzi hizo.
MAHMOUD ABBAS Kenya one huyu alipachikwa jina hili na watangazaji wa soka wa kenya ,huku watangazaji wa Tanzania wakiiga IGA kwa makipa wetu.