DOKEZO Kujiondoa kwa Majeshi ya Africa Kusini nchini Msumbiji na kuiacha Tanzania na Rwanda dhidi ya kundi la kigaidi la Ansar al-Sunna kuna maana gani?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
BTW nina kufahamu, ninaelewa unachokifanya katika mjadala huu.
 
We naona ndio umeingia chaka kabisa. Umeelezea hisia zako kuliko uhalisia wa mambo.

Huo mgogoro sio wa RENAMO na FRELIMO. Hujafatilia mgogoro bali huenda umechukua story za kijiwe cha kahawa
 
Mafuta gani? Mafuta ya mgando ya kupaka mwilini au mafuta gani unayozujgumzia wewe???
Hata hayo ni mafuta pia.

Unafikiri watu wataigombania nchi isiyo yao bure bure?

Wazungu sasa wanatutumia wajinga tuuwane wenyewe kwa wenyewe wakati wao wanajichotea tu. Tukitahamaki, wametumaliza au wameweka vikaragosi vyao.
 
Hata USA na ulaya yote zimekuwa kwa kuharibu Afrika
ushaona nchi za ulaya zinakua kwa kuharibu nchi nyingine!! wao walishajitambua wao ni wamoja saizi vita yao ni dhidi ya waarabu, dhidi ya wachina na dhidi ya waafrica!!

Ni sawa naww utajirike kwa kuwaua wanafamilia yako hiyo ni ugonjwa wa akili
 
BTW nina kufahamu, ninaelewa unachokifanya katika mjadala huu.
Ni kueleza ukweli mchungu ambao watu wengi sana huwa hawapendi kuisikia, hususani jamii za Watu weusi ambao wengi wao ni wanafiki.
We naona ndio umeingia chaka kabisa. Umeelezea hisia zako kuliko uhalisia wa mambo.

Huo mgogoro sio wa RENAMO na FRELIMO. Hujafatilia mgogoro bali huenda umechukua story za kijiwe cha kahawa
Sina kawaida ya kukurupuka, nina uhakika na hicho nilichoeleza.
Msumbiji siyo mbali, unaweza kwenda huko wewe mwenyewe na kisha ukafanya utafiti wako na kujiridhisha juu ya facts za suala hili.
 
Je, Somalia Kuna Mali gani ambayo nchi za Magharibi zinaweza kuchota??
Mkuu inategemea na uelewa wako kuhusu mali!
Kwa ww ni rahisi kudhani mali ni madini na malighafi
Lakin mzungu anapigania zaidi ya mali na malighafi

Vitu ambavyo wazungu wamekua wakipigania

-Kuzigawanya tawala zingine ili wabaki wananguvu
-Kuwapiganisha adui zake na kuwamaliza bila yy kurusha hata siraha
-kupigania maeneo strategic kama mfereji wa suezi,panama nk
-kupigania trade route ( njia za kibiashara)
-Kupigania strategic gate way kama ilivo rwanda ni gateway ya kutorosha madini, south korea,israel gateway ya middle east, na maeneo mengine strategic, somalia gate way ya bahari nyekundu na horn of africa (ndo maana hapa anazikazania nchi kama gdbout ,kenya na ethiopia )
-kupigania malighafi na utajili mfano madin na mafuta


Hivo ndugu yangu panua fikra
 
Umejuaje kama sipo Msumbiji?
 
kenge hao walifurushwa kimyakimya bila kutajwa kuwa ni magaidi. Hivi waliichukuliaje tanzania, waliona ni kama congo mashariki? Walijitoa ufahamu wakaona kibiti wanaweza kuweka kambi huko bila kushughulikiwa. Tz sio msumbiji, mipaka yake si ya kuvamiwa na wahuni wa aina yeyote
 
Hawa wapumbavu wa jwtz wanaogombea na na raia kwenye bar huko mitaani kila siku si wapelekwe huko Msumbiji ?
Au jwtz/ jeshi la wapumbav Tanzania ni jeshi la kufuga vitambi na makalio kuja kugombania pombe na malaya mitaani ?
heshimu jeshi la nchi yako, wana kazi nzito sana kulinda nchi
 
Ukichunguza kwa umakini Sana utagundua kwamba yale maeneo karibia yote yenye vurugu kule Msumbiji yana historia kongwe sana kuhusiana na suala la vurugu za kisiasa, hata kabla ya Taifa hilo la Msumbiji halijapata uhuru wake kutoka kwa mkoloni wao Ureno. Kambi nyingi sana za Makundi ya kisiasa ya Wapigania Uhuru wa nchi hiyo ya Msumbiji ziliwekwa katika ukanda huo wa Kaskazini mwa nchi hiyo, maeneo ambayo hadi leo hii bado yanaendelea kukumbwa na vurugu. Makundi ya Wapigania Uhuru ya vyama vya Siasa vya FRELIMO na RENAMO vilikuwa na Kambi zao nyingi za wazi na za siri kubwa ktk maeneo hayo yenye vurugu kwa sasa. Baada ya kufanikisha suala la kuuangusha utawala wa mkoloni wao Ureno, maeneo hayo tayari yalikuwa yamevurugwa vibaya sana na vita vya ukombozi, miundombinu yote ya kujenga uchumi kama vile viwanda viliharabiwa kabisa na mapigano ya vita.
Mbaya zaidi, hata chama cha Siasa cha FRELIMO kilipofanikiwa kushika madaraka ktk nchi hiyo ya Msumbiji, haikukishirikisha Chama cha RENAMO ktk kuitawala nchi hiyo ya Msumbiji, badala yake vyama hivyo viligawanyika na kuwa vyama vinavyohasimiana, vikapigana vita tena wao kwa wao ili kugombea kupata udhibiti wa madaraka ktk nchi hiyo, hatimaye Chama cha RENAMO kilizidiwa nguvu na kushindwa vita. Chama cha FRELIMO kutokana na msaada mkubwa waliopata kutoka kwa Mwl. J. K. Nyerere na CCM yake, walifanikiwa kuhodhi na kudhibiti mamlaka na madaraka yote ya nchi hiyo ya Msumbiji, na RENAMO kikawa Chama kikuu cha Upinzani dhidi ya FRELIMO.
Mbaya zaidi tena, utawala wa FRELIMO ulikichukulia Chama cha RENAMO kama Kundi la Waasi wala siyo Chama cha Siasa, Matokeo yake Wanachama na Wapiganaji wa RENAMO wakakimbilia msituni na kuweka Kambi zao nyingi za Siri kwenye huo Upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Msumbiji.

Serikali ya Msumbiji Kama ililitelekeza kabisa kwa muda mrefu eneo hilo lililopo Kaskazini mwa nchi hiyo kwa sababu ililiona kama eneo lenye maficho ya Waasi wa RENAMO, hata huduma za kijamii zilikuwa duni sana kwenye maeneo hayo. Wananchi wengi wa upande huo wa Kaskazini mwa nchi waliona kama Serikali ya Msumbiji imewatenga na haikuwa inawajali. Serikali ilijichimbia mizizi kwenye eneo la Kusini mwa nchi hiyo ya Msumbiji na kuigawa nchi ktk mapande mawili ya Kaskazini na Kusini. Serikali hiyo ya Msumbiji ilirudi tena kwa kasi upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya Ugunduzi wa Nishati ya Gesi kwenye maeneo hayo ya Kaskazini, hapo ndipo ukawa mwanzo mpya wa kuibuka kwa Vurugu hizi zinazoendelea hivi sasa ktk eneo hilo la Kaskazini mwa nchi hiyo ya Msumbiji.

Suala la Dini au Udini ktk vurugu hizo za huko Msumbiji linatumika tu na wahusika kama "SCAPEGOAT" ili kuweza kupata msaada wa kijeshi na wa silaha za kupigania vita dhidi ya maadui zao.
 
Hicho kikundi cha msumbiji umeita CHA KIISLAMU, vipi M23 ni kikundi cha akina nani? Sometime muwe mnatumia common sense na sio utumbo kufikiri
 
Anzeni kuikalia Zanzibar Kwanza kimabavu ndio muwe na ndoto za kutanua mipaka ya nchi,hamuoni huu muungano umeshazeeka kinachotakiwa hapo sio kuuvunja Bali ni Zanzibar kulazimishwa kumezwa na bara? Akigoma achakazwe. Tuanze na tunayemumudu Kwanza.
 
Heshi letu linatosha. Wachangie bajeti ya ulinzi tu tugawe ajira kwa vijana wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…