Kujipanga kwa uchaguzi mkuu 2020

Kujipanga kwa uchaguzi mkuu 2020

DITOPILE WAPILI

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
384
Reaction score
261
Sasa ni muda muafaka kwa vyama vya siasa, kupitia kwa hatua ya mwisho kabla ya kwenda kunadi SERA NA ILANI ZA UCHAGUZI 2020 za vyama zao.

Hii itasaidia wananchi kupata SERA ZILIZO SHIBA, hivyo kutakuwa na wigo mpana wa kuchagua sera bora kutoka vyama mbalimbali vya siasa,

Kuliko sera na ilani za kuungaunga (ujanja ujanja), yaani chama hakitaki kujipanga nn kitaenda kusema au kutoa sera zake eti hadi kisikie chama fulani kimesema hivi ndiyo kesho yake kinakuja na sera zake.

Siasa za ulaghai mwisho wake ni anguko kubwa la kisiasa kama sio kufa kwa chama hicho.

Chama kitakacho jipanga na kuandaai sera zake mapema kwa wananchi, basi wananchi watapata fursa ya kuwaelewa kupata wafuasi na kura nyingi.

Hata kama mikutano ya hadhara imepigwa marufuku, vizuri kuhakikisha vingozi na wafuasi wa chama chako wanaelewe MISSION na VISION ya chama chao, hivyo watabaki na kuwa mabalozi wazuri wa chama chao katika maeneo yao.

Wananchi wanataka kujua utawafanyia nini? sio kwenda jukwaa na kuporomosha mitusi, kashfa na kubeza vyama vingine.

Kwa vyama vilivyojipanga kwenda kulilia kwa wananchi ili wapate huruma ya wananchi SIDHANI KAMA MBINU HII ITAWASAIDIA KUPATA KURA ZA KUTOSHA.
 
CCM ni mabingwa wa kupanga sera na kutoa ahadi lakini utekelezaji sifuri. Wapinzani tunataka tume huru wananchi waamue.
 
CCM ni mabingwa wa kupanga sera na kutoa ahadi lakini utekelezaji sifuri. Wapinzani tunataka tume huru wananchi waamue.
Kikubwa wanachotaka CCM ni ushindi tu, wanao subiri usafiri wa meli stend ya mabasi ubungo watasubiri milele!
 
Back
Top Bottom