Mkuu katika hali ya kawaida inapaswa kupeana mali au hela mbele ya mashahidi waaminifu au maandishi yatakayo onyesha juu ya hayo makabidhiano kwa sababu mbali na kudhulumiana kinaweza kutokea chochote mfano miongoni mwenu mmoja akafariki au akaugua mahututi au akafungwa au jambo lolote likatokea hapo ndipo wale mashahidi au maandishi husaidia ili kupata haki yako.
Kuhusu kadhia yako, kama imeshindiana kulipwa pesa au mali yako basi fuata mkondo wa sheria mfano anza kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa naye atakupa muongozo kama uende polisi au laa.
Lakini kabla hujachukua hiyo hatua jaribu sana kutengeneza ushahidi wa kukulinda maana bila ushahidi anaweza kukuruka kwamba hukumpa mali, jaribu kufanya hivi; nenda na smart phone huku umeweka record mode kwa siri, na utakapofika kwa huyo mdeni wako umsalimie na umuulize juu ya hilo deni kwamba atakulipa lini atakapojibu maneno yako na yake yatakuwa yamerikodiwa humo ndani basi hayo majibu yake yatakuwa ni ushahidi wa kukiri kwake kama unamdai-- hiyo kwa kiasi fulani inaweza kukusaidia kupata haki yako mbele ya vyombo sheria ambavyo mara nyingi hutaka ushahidi.