Kujipendelea Muhimu

Kujipendelea Muhimu

Sikujui nikupe nini Mbu,post yako ni nzuri sana,tena sana ngoja nimtafute muhusika naye ajisomee.

...asante yanitosha mie, mhusika asijenuna akiisoma hiyo 'nikupe nini Mbu!' LOL...Enjoy!

Yeah, we all want to do this for our wives/husbands, to re-kindle our love
But, truly, an innocent Tanzanian salary man/woman can afford this luxury?
I doubt, may be, after saving for a life time!!
Cheers!

Futota. YES WE CAN bana...kwanini isiwezekane?
Tatizo la kuwa 'Pessimist,' ni kujipa uzito wa 'kuangalia nje ya Boksi!'

  • Chukulia, Mwaka mzima umetoa Michango ya harusi kiasi gani,
  • Unakwenda baa na washkaji (sio Mke) mara ngapi na una spend kiasi gani kila wiki...
  • Unatumia gharama kiasi gani kwa matumizi ya kujikweza pasipo na ulazima...mfano kuhonga!
Tatizo jingine, wengi wetu tunashindwa kujipangia mipango ya muda mrefu. Kama imewezekana kwa Wachagga kufanya Annual Migration kila Christmas kwenda Uchagani, iweje sie makabila ya pwani tuishie kucheza Gombe Sugu na mdundiko siku saba huku tukiwalisha na kuwanywesha watu baki, eti tunasafisha jina?

Tuanzeni uchoyo wa fikra.
Tuanzie kujipendelea, (priority) ni wewe na Mkeo kwanza.
 
Hahahahah lol! MR zipo sana hizo! We Baba nanihii lakini huku sikufuja hela? Kile kibanda tutamaliza lini? Hii hela tunayotumia hapa ni sawa na mifuko mingapi ya saruji!?.....Kujirusha mwiko mpaka kibanda kiishe!!!

Unakuta mtu mzima umelipia mkae siku tatu halafu unaanza pewa lecture kama hizo...mwishoe waulizwa siku tatu zote za nini naomba twende ukaombe wakurudishie hela ya siku mbili turudi nyumbani.halafu haya mambo ya kuchukua hela benki bila kunishirikisha mi sipendi kabisa.
 
Mbu aksante kwa Remainder nzuri kama hii. Duh kama unamfanyia hayo umpendae mbona namwonea wivu!

Ngoja na mimi nitafute wa kumshika mkono nimlete aje asome hapa kama alivyofanya chauro.

MR umenichekesha sana wanawake wengine tunajifanyaga tuna uchungu na maendeleo kuliko wanaume na cha ajabu ni kuwa hatuzipigii kelele zile zinazotumbuliwa karibu kila siku Baba Chanja kwenye viti virefu akizungusha rounds za bia, konyagi, value, JDs; rounds za nyama choma na mafuta ya gari maana viti vingine huwa vinafuatwa mpaka nje ya mji!

Mbu aksante

Mwj1 hapo penye wekundu umesema yote. Huo ni ukweli usiopingika.
Kuna watu wanagharamikia Nyumba ndogo mpaka washkaji tunaona kufuru!...

Wewe una mtritigi? kwa kweli mambo kama haya yanaongeza sana mapenzi basi tu hatujagundua, i wish ......

Swali lako zuri ila nikikujibu ndio nitakuwa najikweza. Kuileta mada hii hadharani ni uthibitisho wa kile ninachokifikiria. Majibu mengine acha tu 'yafunikiwe kombe mwanaharamu apite!'
 
Mwj1 hapo penye wekundu umesema yote. Huo ni ukweli usiopingika.
Kuna watu wanagharamikia Nyumba ndogo mpaka washkaji tunaona kufuru!...
Ehee?!! kumbe wanafaidi sana wenzetu.................................Hamna mtu anayetafuta nyumba ndogo humu jamani? Mkinionea mnijuze. Natanguliza aksante.

Swali lako zuri ila nikikujibu ndio nitakuwa najikweza. Kuileta mada hii hadharani ni uthibitisho wa kile ninachokifikiria. Majibu mengine acha tu 'yafunikiwe kombe mwanaharamu apite!'

Mbu una mafumbo kama mwalimu wa kiswahili!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Unajua vitu vingine hatuviwazagi basi akitokea mtu akakupa mawazo mbadala huna budi kumshukuru.

...asante yanitosha mie, mhusika asijenuna akiisoma hiyo 'nikupe nini Mbu!' LOL...Enjoy!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
mkuu wapi hapo?

Tanzania hii bana, Tembea ujionee...

Picha ya juu ni Serengeti Plains....Kirawira, Seronera, Serengeti Serena unapata mandhari kama hiyo.
Picha inayofuatia ni Pwani ya Zanzibar....lakini pia Bagamoyo waweza pata mandhari kama hiyo
Picha ya tatu ni Ngorongoro...kwa mbali (chini) unaona mandhari nzuri ya Crater.

Picha ya Mwisho chini ni kusini mwa Tanzania,....Selous Game reserve...unapata viburudisho vya namna hii;

17816-suite-the-retreat-selous-and-southern-tanzania-tanzania.jpg

nikipelekwa kwenye hiyo picha ya mwisho namzalia mtu kabisaaaaaaaaa

...ha ha ha!, BB mambo si ndio hayo bana.
Ni haki yako ya msingi kila baada muda kumsisitiza mumeo mkafanye 'semina elekezi' mambo yaliyotekelezeka
na yanayohitaji msukumo mpya kwa zile ahadi mlizopeana kwenye honeymoon.
 
Nice thread... Ila mkuu, umetulenga wanaume kwa sana mbn? Nadhan hata wake zetu nao wanapaswa kututoa maeneo kama haya.. Hasa ukizingatia mifuko yetu mara nyingi ipo kimaendeleo zaidi...
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Jamani mbona wengine tumeshaanza siku nyingi????????Ukisubiri mpaka hela zijae mifukoni mpaka zimwagike chini raha kama hizo hutaziona kamwe maishani mwako. Kama una kibanda, kausafiri (ka-RAV4), vitoto vipo kwa mama Rwakatare, basi anza kula raha. Mimi naona hivyo
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Unakuta mtu mzima umelipia mkae siku tatu halafu unaanza pewa lecture kama hizo...mwishoe waulizwa siku tatu zote za nini naomba twende ukaombe wakurudishie hela ya siku mbili turudi nyumbani.halafu haya mambo ya kuchukua hela benki bila kunishirikisha mi sipendi kabisa.

Sangara yeshakukumba wewe, ha ha ha! Nimekusoma neno kwa neno,
hiyo ndio sababu wengine hujonea bora kuziunguza na 'nyumba ndogo' kuliko kujikera bure!

Ehee?!! kumbe wanafaidi sana wenzetu.................................Hamna mtu anayetafuta nyumba ndogo humu jamani? Mkinionea mnijuze. Natanguliza aksante.

Mbu una mafumbo kama mwalimu wa kiswahili!!

Mwj1 la aziz wangu,....Nakushauri urudi page one ukamsome tena Maria Roza kisha urudie walichokiandika kina BaK, Fidel80, na Sangara! Nyumba ndogo wanafwaudu kwakuwa Nyumba kubwa hawaishi Gubu!

Kiswahili naringia kwetu pwani mie...he he!

Nice thread... Ila mkuu, umetulenga wanaume kwa sana mbn? Nadhan hata wake zetu nao wanapaswa kututoa maeneo kama haya.. Hasa ukizingatia mifuko yetu mara nyingi ipo kimaendeleo zaidi...

Avatar pole kwa kukukwaza bro,...natamani kusema lililo rohoni lakini acha thread isoge sogee kidogo...soon nitawashukia na wao!
 
Jamani mbona wengine tumeshaanza siku nyingi????????Ukisubiri mpaka hela zijae mifukoni mpaka zimwagike chini raha kama hizo hutaziona kamwe maishani mwako. Kama una kibanda, kausafiri (ka-RAV4), vitoto vipo kwa mama Rwakatare, basi anza kula raha. Mimi naona hivyo

Nice one Fugwe. Maishani, raha ujipe mwenyewe ati!
 
duh, hii nimeikubali.

Baadhi ya wanaume wanapenda kuspend hivi na mipango ya kando. Dont know why.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Avatar pole kwa kukukwaza bro,...natamani kusema lililo rohoni lakini acha thread isoge sogee kidogo...soon nitawashukia na wao![/COLOR][/SIZE][/FONT]
Washukie tuone watakavyo react!..
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
duh, hii nimeikubali.

Baadhi ya wanaume wanapenda kuspend hivi na mipango ya kando. Dont know why.

Freema, rudia page One kumsoma Maria Roza, Bubu Ataka Kusema, ...na Sangara.
Wametoa majibu ya msingi kabisa mydear.
 
Haya ndio mambo nayoyapenda kuliko kitu chochote, hata nikiwa alone nasoma novel poa tu, mie napenda sana kusafiri
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Tanzania hii bana, Tembea ujionee...

Picha ya juu ni Serengeti Plains....Kirawira, Seronera, Serengeti Serena unapata mandhari kama hiyo.
Picha inayofuatia ni Pwani ya Zanzibar....lakini pia Bagamoyo waweza pata mandhari kama hiyo
Picha ya tatu ni Ngorongoro...kwa mbali (chini) unaona mandhari nzuri ya Crater.

Picha ya Mwisho chini ni kusini mwa Tanzania,....Selous Game reserve...unapata viburudisho vya namna hii;

17816-suite-the-retreat-selous-and-southern-tanzania-tanzania.jpg

...ha ha ha!, BB mambo si ndio hayo bana.
Ni haki yako ya msingi kila baada muda kumsisitiza mumeo mkafanye 'semina elekezi' mambo yaliyotekelezeka
na yanayohitaji msukumo mpya kwa zile ahadi mlizopeana kwenye honeymoon.
Hicho kitanda kinaitwa victoria bed we acha tu
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Code:
Kwa wale wenzangu na mie ambao tukishanuniwa ndio 'hakieleweki mpaka anunuliwe khanga,' si vibaya tukajitutumua na kum-surprise mother house na bonge la week end 'Romantic' retreats kama hizi angalau mara moja kwa mwaka jamani...

never waste time buying love..it has never worked and it will never do........................elekeza hizi nguvu katika kuonyesha mapenzi ya kweli siyo ya vitu,.................................................acha kumsononesha mwenzio kwa matarajio ya kuwa utampooza kwa vitu au mavituz...........
 
Back
Top Bottom