SoC03 Kujitambua

SoC03 Kujitambua

Stories of Change - 2023 Competition

Petro Masunga

Member
Joined
May 5, 2023
Posts
7
Reaction score
7
Kuna umuhimu mkubwa sana wa sisi, kuacha kutazama picha, ili tupate mwelekeo. Bali sisi wenyewe ndiyo tuwe hiyo picha. Nyumba iliyo chafu, hata ukileta vitu Safi ndani yake, bado itaendelea kuwa chafu tu. Maana yake, kujifunza kwa wengine ni vizuri, lakini itafaa sana, kama utaisafisha kwanza hiyo nyumba, ndiyo ulete hivyo vitu Safi. Mfano huu, ni kwa kila sekta, ikiongozwa na mtu binafsi. Ni uwajibikaji kwa ajili ya kuijenga nchi yetu. Ninapenda kusema kwamba, tuko hapa siyo kwa bahati mbaya, la. Bali kila mmoja wetu ako na kitu cha ziada kwa ajili ya ulimwengu, na kwa ajili ya nchi yake. Hivyo kujitambua kwako, kutakufanya usipoteze muda kwa ajili ya vitu visivyokuwa na maana. Mwelekeo mzuri wa kuijenga nchi yetu ni lazima kila mmoja wetu ajitambue, na nini kina mpasa kama binadamu kamili.
Asante!
 
Upvote 3
Back
Top Bottom