KUJITAWALA: Hatua 21 za Kuwa Mwanasiasa Mkubwa kwa Karne ya 21

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
KUJITAWALA: Hatua 21 za Kuwa Mwanasiasa Mkubwa kwa Karne ya 21
Mtunzi; Robert Heriel
+255693322300

Hatua ya 4:
FANYA MAZOEZI YA UJASIRI WA KUJIELEZA.

4.1 Sauti Yako Ni Sauti Ya Taifa

Kama huwezi kusema unachofikiri kwa ujasiri na kwa heshima, basi huwezi kuongoza taifa. Sauti ya kiongozi ni silaha ya kwanza ya mabadiliko. Lakini ili iwe silaha ya kweli, lazima ifundishwe, ifanyiwe mazoezi, na ikomae ndani Kwa ujasiri wa dhati.

4.2 Ujasiri Hauzaliwi – Hujengwa

Watu wengi hudhani kuwa kiongozi mzuri huzaliwa akiwa na kipawa cha kuongea.
Lakini ukweli ni kwamba, speaking confidence is a muscle, unalijenga kadri unavyolizungumza.
Unaweza kuwa na maono mazuri, elimu kubwa, lakini kama huwezi kuyasema kwa watu kwa ufasaha, yatabaki kichwani kwako.

4.3 Lugha ya Uongozi Inahitaji Mazoezi

Unahitaji kujua:

Unasema nini?

Kwa nini unasema hivyo?

Kwa namna gani itafika kwa watu?

Na itawagusa vipi kihisia, kiakili na kitabia?

Kiongozi mzuri hatoi hotuba ya kupendeza, anatoa ujumbe wa kugusa hisia, kubadili fikra na kuleta mabadiliko ya tabia.

4.4 Aina Tatu za Uwasilishaji wa Kiongozi

i. Speaking to Convince (Kushawishi)
Unapozungumza ili kugeuza fikra. Hii ni muhimu sana wakati wa kampeni, mijadala au midahalo. Kama unavyojua Kwa sasa dunia inaenda kwenye mfumo wa demokrasia. Mwenye ujuzi wa kushawishi na kubadilisha fikra za watu wengi huyo ndiye Kiongozi atakayechaguliwa.

ii. Speaking to Inform (Kufundisha)
Hapa unaelimisha. Unatoa data, mifano, historia, sheria. Hii ni muhimu kwa wanasiasa watunga sera.

iii. Speaking to Inspire (Kuhamasisha)
Unatoa hotuba yenye moto wa mabadiliko. Unawasha matumaini. Hapa unahitaji passion + message clarity.

4.5 Jifunze Kuongea Kwa Lugha ya Watu wa Kawaida/mtaani.
Siasa ya kweli haipo kwenye lugha ngumu.
Kiongozi wa karne hii lazima awe na uwezo wa kusema jambo gumu kwa lugha rahisi, kutoka technical language kwenda people language.

Mfano:
Badala ya kusema “sera ya uwezeshaji wa vijana”, sema “tutatoa mikopo na mafunzo ili vijana wawe na biashara zao.”
Wakati mwingine kusema Sera au lugha za kitaaluma zinapunguza nguvu Kwa watu wa kawaida wa mtaani

4.6 Mbinu za Kujieleza

i. Soma Kwa Sauti ya Juu (Reading Aloud)
Chagua hotuba nzuri ya kisiasa, isome kwa sauti, mbele ya kioo au rafiki.
Fuatilia tone, usikivu, na miondoko ya maneno.

ii. Rekodi Hotuba Zako Fupi
Tumia simu yako. Ongea dakika 2 juu ya mada fulani ya kijamii.
Halafu jisikilize. Angalia kasoro zako, ongea tena kwa ubora zaidi.

iii. Shiriki katika vikundi vya Majadiliano
Anza na watu wachache, toa maoni yako.
Kadri unavyotoa moani , ndivyo unavyokua.
Speaking is like a fire, it grows when you feed it.

4.7 Mbinu za Kupunguza Hofu ya Kuongea Mbele ya Watu

I. Jifunze kujitayarisha mapema

Ii. Fanya “deep breathing” kabla hujasimama

Iii. Angalia watu moja kwa moja (eye contact)

iv. Tumia mifano ya kweli au ya maisha yako

v. Usilazimishe kiswahili kigumu Cha kitaalamu, ongea kwa lugha rahisi

vi. Kuwa wewe, authenticity sells more than perfection.

4.8 Ujasiri wa Kujieleza ni Silaha ya Maamuzi
Kiongozi asiyeweza kujieleza kwa usahihi, huamua kwa hofu.
Lakini kiongozi anayezungumza kwa ujasiri, huongoza kwa hoja.
Hii ndiyo sababu watu wengi huamua kumuunga mkono mtu wanaomsikiliza, si tu anayejulikana.

4.9 Homework; Jichunguze! Ukijiuliza;
1. Nimesimama lini mara ya mwisho kuzungumza mbele ya watu?

2. Je, naweza kueleza maono yangu kwa dakika mbili bila kukosea?
3. Naweza kuongea bila kutegemea kuangalia karatasi?

4. Ninasikiliza watu nikiwa nimesimama mbele

“Sauti ya kiongozi haipo tu mdomoni, ipo kwenye ujasiri wake wa kusema ukweli.”
– Robert Heriel

Hiyo ni sehemu katika kitabu Cha KUJITAWALA: Hatua 21 za Kuwa Mwanasiasa Mkubwa kwa Karne ya 21.

Kitabu hiki Bei yake ni Tsh 20,000/=
Kinatolewa Kwa oda.
Unatuma pesa ndani ya siku saba unapata kitabu. Hii ni Kwa sababu tunachapisha Kwa Oda. Kila oda Mia tunatoa. Siku saba zinatosha kupata oda hizo.

Namba ya muamala
+255758216209
M- PESA
Robert Heriel

Ukishatuma utantumia ujumbe jina la Wakala au namba uliyotumia kutuma pesa.
file_00000000fa3861f99e8e57575aac2125.png
 
Politics has no taught
Hawa mzee huwa wanaibuka tu tena wanakuwa wamoto kweli kweli
Sijajua huwa wanaandaliwa saa ngapi?
Hawa wanaondaliwa vyuoni ni wataalamu ndio hao wanakuja kuwasupport hao walioibuka
 
Haujui chochote na hapa wazungu watatawatalala milele kwakuwa wanasoma Sana
 
Unless hujui kutawala ni nini?

Kutawala ni dhana pana sana

Kwa taarifa yako tu kuna watu hawajui hata kuongea kusimama vizuri na kuvaa kaunda suti

Lakini wanatawala kila kitu usikute hata hao unaowaita watawala huenda kwao kupata accessories and gadgets za kukutawala

Do not fantasise politics as if kila mtu bila hiyo hamna maisha

Tujifunze kutawala fahamu na utu wetu tutakuwa watu bora sana na tutafaa hata kuwatawala wengine
 
Kuna post nyingine unaziacha Mimi sipendi watu much know ambao ni lay man Ila wanakuwa so bitter kwa kila jambo
 
Politics has no taught
Hawa mzee huwa wanaibuka tu tena wanakuwa wamoto kweli kweli
Sijajua huwa wanaandaliwa saa ngapi?
Hawa wanaondaliwa vyuoni ni wataalamu ndio hao wanakuja kuwasupport hao walioibuka

Mkuu tunazungunzia mwanasiasa mkubwa mwenye viwango vya kitaifa na kimataifa
 
KUJITAWALA: Hatua 21 za Kuwa Mwanasiasa Mkubwa kwa Karne ya 21
Mtunzi; Robert Heriel
+255693322300

Hatua ya 4:
FANYA MAZOEZI YA UJASIRI WA KUJIELEZA.

4.1 Sauti Yako Ni Sauti Ya Taifa

Kama huwezi kusema unachofikiri kwa ujasiri na kwa heshima, basi huwezi kuongoza taifa. Sauti ya kiongozi ni silaha ya kwanza ya mabadiliko. Lakini ili iwe silaha ya kweli, lazima ifundishwe, ifanyiwe mazoezi, na ikomae ndani Kwa ujasiri wa dhati.

4.2 Ujasiri Hauzaliwi – Hujengwa

Watu wengi hudhani kuwa kiongozi mzuri huzaliwa akiwa na kipawa cha kuongea.
Lakini ukweli ni kwamba, speaking confidence is a muscle, unalijenga kadri unavyolizungumza.
Unaweza kuwa na maono mazuri, elimu kubwa, lakini kama huwezi kuyasema kwa watu kwa ufasaha, yatabaki kichwani kwako.

4.3 Lugha ya Uongozi Inahitaji Mazoezi

Unahitaji kujua:

Unasema nini?

Kwa nini unasema hivyo?

Kwa namna gani itafika kwa watu?

Na itawagusa vipi kihisia, kiakili na kitabia?

Kiongozi mzuri hatoi hotuba ya kupendeza, anatoa ujumbe wa kugusa hisia, kubadili fikra na kuleta mabadiliko ya tabia.

4.4 Aina Tatu za Uwasilishaji wa Kiongozi

i. Speaking to Convince (Kushawishi)
Unapozungumza ili kugeuza fikra. Hii ni muhimu sana wakati wa kampeni, mijadala au midahalo. Kama unavyojua Kwa sasa dunia inaenda kwenye mfumo wa demokrasia. Mwenye ujuzi wa kushawishi na kubadilisha fikra za watu wengi huyo ndiye Kiongozi atakayechaguliwa.

ii. Speaking to Inform (Kufundisha)
Hapa unaelimisha. Unatoa data, mifano, historia, sheria. Hii ni muhimu kwa wanasiasa watunga sera.

iii. Speaking to Inspire (Kuhamasisha)
Unatoa hotuba yenye moto wa mabadiliko. Unawasha matumaini. Hapa unahitaji passion + message clarity.

4.5 Jifunze Kuongea Kwa Lugha ya Watu wa Kawaida/mtaani.
Siasa ya kweli haipo kwenye lugha ngumu.
Kiongozi wa karne hii lazima awe na uwezo wa kusema jambo gumu kwa lugha rahisi, kutoka technical language kwenda people language.

Mfano:
Badala ya kusema “sera ya uwezeshaji wa vijana”, sema “tutatoa mikopo na mafunzo ili vijana wawe na biashara zao.”
Wakati mwingine kusema Sera au lugha za kitaaluma zinapunguza nguvu Kwa watu wa kawaida wa mtaani

4.6 Mbinu za Kujieleza

i. Soma Kwa Sauti ya Juu (Reading Aloud)
Chagua hotuba nzuri ya kisiasa, isome kwa sauti, mbele ya kioo au rafiki.
Fuatilia tone, usikivu, na miondoko ya maneno.

ii. Rekodi Hotuba Zako Fupi
Tumia simu yako. Ongea dakika 2 juu ya mada fulani ya kijamii.
Halafu jisikilize. Angalia kasoro zako, ongea tena kwa ubora zaidi.

iii. Shiriki katika vikundi vya Majadiliano
Anza na watu wachache, toa maoni yako.
Kadri unavyotoa moani , ndivyo unavyokua.
Speaking is like a fire, it grows when you feed it.

4.7 Mbinu za Kupunguza Hofu ya Kuongea Mbele ya Watu

I. Jifunze kujitayarisha mapema

Ii. Fanya “deep breathing” kabla hujasimama

Iii. Angalia watu moja kwa moja (eye contact)

iv. Tumia mifano ya kweli au ya maisha yako

v. Usilazimishe kiswahili kigumu Cha kitaalamu, ongea kwa lugha rahisi

vi. Kuwa wewe, authenticity sells more than perfection.

4.8 Ujasiri wa Kujieleza ni Silaha ya Maamuzi
Kiongozi asiyeweza kujieleza kwa usahihi, huamua kwa hofu.
Lakini kiongozi anayezungumza kwa ujasiri, huongoza kwa hoja.
Hii ndiyo sababu watu wengi huamua kumuunga mkono mtu wanaomsikiliza, si tu anayejulikana.

4.9 Homework; Jichunguze! Ukijiuliza;
1. Nimesimama lini mara ya mwisho kuzungumza mbele ya watu?

2. Je, naweza kueleza maono yangu kwa dakika mbili bila kukosea?
3. Naweza kuongea bila kutegemea kuangalia karatasi?

4. Ninasikiliza watu nikiwa nimesimama mbele

“Sauti ya kiongozi haipo tu mdomoni, ipo kwenye ujasiri wake wa kusema ukweli.”
– Robert Heriel

Hiyo ni sehemu katika kitabu Cha KUJITAWALA: Hatua 21 za Kuwa Mwanasiasa Mkubwa kwa Karne ya 21.

Kitabu hiki Bei yake ni Tsh 20,000/=
Kinatolewa Kwa oda.
Unatuma pesa ndani ya siku saba unapata kitabu. Hii ni Kwa sababu tunachapisha Kwa Oda. Kila oda Mia tunatoa. Siku saba zinatosha kupata oda hizo.

Namba ya muamala
+255758216209
M- PESA
Robert Heriel

Ukishatuma utantumia ujumbe jina la Wakala au namba uliyotumia kutuma pesa.View attachment 3403730
Soft copy inapatikana kwa bei gani?
 
Back
Top Bottom