SoC04 Kujitegemea kwa nafasi za ajira zinazopatikana kutokea kwa watumishi waliostaafu na waliofariki

SoC04 Kujitegemea kwa nafasi za ajira zinazopatikana kutokea kwa watumishi waliostaafu na waliofariki

Tanzania Tuitakayo competition threads

changae2020

New Member
Joined
Jun 6, 2024
Posts
1
Reaction score
0
KUJITEGEMEA KWA NAFASI ZA AJIRA ZINAZOPATIKANA KUTOKEA KWA WATUMISHI WALIOSTAAFUU NA WALIOFARIKI.

Kupata kazi au ajira baada ya kumaliza masomo imekuwa ni ndoto ya kila msomi, lakini katika karne hii hasa miaka ya hivi karibuni ndoto hii imekuwa ikitimia kwa wachache miongoni mwa wengi. Hali hii imesababishwa na kuongezeka kwa idadi kubwa ya wasomi ukilinganisha na nafasi za ajira zinazotolewa na serikali na zile zilizopo nchini.

Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili kukabiliana na tatizo hili mfano serikali imefikira kufanya maboresho mbalimbali katika sekta mama ya elimu, ikiwemo yale yanayohusu mfumo mzima wa elimu na yale yanayohusu mitaala ya elimu ili kuweza kuzalisha wasomi watakao weza kuwa na ujuzi ambao utawasaidia wenyewe kuwa tegemezi kwa kujiajiri wenyewe kutoka kwenye kutegemea ajira serikalini peke yake.

Serikali pia imeendelea kutoa nafasi mbalimbali za ajira katika sekta zake mfano elimu, afya, ulinzi bila kusahau kubuni njia nyingine za kuwasaidia vijana wa kitanzania ili waongeze ujuzi na kuweza kujiajiri wenyewe kupitia mpango wake wa kufadhili mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana watakao soma katika vyuo hivyo vya ufundi stadi.

Vijana kwa upande wao wamekuwa wakizitumia fursa hizo zinazotolewa na serikali kutokea kule kwenye elimu, Afya bila kusahau zile za jeshi japo kwa uchache wa fursa hizo. serikali haiwezi kuajiri watu wote ambao wameshahitimu masomo yao ila serikali inao uwezo wa kubuni sera na mipango bila kusahau kutenegeneza mazingira mazuri endelevu yatakayo wapatia vijana na wasomi ajira za kudumu.

Baadhi ya ajira zinazopatikana kutoka kwenye miradi mbalimbali ya serikali, Imekuwa ikitoa fursa za ajira chache za kudumu au za muda mrefu na nyingi zisizo za kudumu au za muda mfupi, ambapo miradi hiyo ikishakamilika zile ajira nyingi za muda mfupi nazo humalizika na tatizo la ajira kurudi tena pale pale miongoni mwa wengi. Mawazo yangu ni katika kuangalia uwezekano wa serikali kutafuta njia mbadala katika kuongeza nafasi za ajira nchini ili kutatua tatizo hili la ajira linalozidi kuongezeka kutokana na wasomi wasio na ajira kuzidi kuongezeka nchini.

Fikra zangu zimefikiria uwezekano wa kuwepo kwa fungu la ajira litakalo jitegemea kutokea kwenye nafasi za ajira zinazopatikana kutoka kwa watumishi waliostaafu na waliofariki, kwa maana nafasi hizo zisijumuishwe kwenye kundi la ajira linalotolewa na serikali katika miaka mbalimbali ya fedha kama tulivyozoea yakitangazwa bungeni katika uwasilishwaji wa bajeti mbalimbali za serikali.

Ila kuwepo na kundi jipya ambalo litatokana na nafasi zinazoachwa na watumishi wa serikali wanaostaafu na kufariki kwenye wizara mbalimbali za serikali, ili nafasi hizo zibadilishwe kuwa nafasi za ajira zitakazo tangazwa na serikali kama nafasi nyingine za ajira. kuwepo kwa makundi mawili ya nafasi za ajira yatasaidia kuongeza nafasi za ajira nchini.

Jambo hili linaweza kufanyika ndani ya miaka mitano mpaka kumi, ambapo ndani ya miaka mitano serikali inao uwezo wa kupata taarifa za watumishi wa serikali waliostaafu na waliofariki kutoka kwenye sekta na wizara mbalimbali za serikali ili kupata idadi kamili ya watumishi hao ndani ya miaka hiyo. kila sekta na wizara inao wafanyakazi ambao wanastaafu na wanafariki, kwa namna hiyo kila sekta na wizara ya serikali lazima itahitaji wafanyakazi wengine ili iweze kuziba nafasi zilizoachwa na wafanyakazi hao ambao kwa wakati huo hawatakuwepo kwenye nafasi hizo.

Uzuri ni kwamba mfumo wa usawa ni muhimu zaidi katika kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi, mfumo huu ni ule unao tengeneza mazingira endelevu na imara ya kuendelea kufanya kazi kwa ubora na ufanisi uleule, sasa kunapokuwepo na mapungufu ya wafanyakazi katika sekta fulani mfano elimu, shule au Afya, hospitali kutokana na upungufu wa wafanyakazi ambao walistaafu au kufariki bila kuongeza wafanyakazi wapya maana yake unaathiri ubora wa utoaji wa huduma za jamii kwa wananchi ambao ulikuwepo wakati watumishi hao wapo.

Serikali inajenga shule, hospitali, zahanati lakini je, wafanyakazi wanaokwenda kufanya kazi kwenye vituo hivi ni wapya au wanatolewa kutoka vituo vingine? jibu ni kwamba wapo wanaotolewa kutoka vituo vingine na kupelekwa vituo hivi vipya huku vituo vya zamani vikibaki na uchache wa wafanyakazi na hata vile vipya havijitoshelezi, mfano Zahanati “c” ni kituo kipya cha serikali ambacho kinahitaji wafanyakazi ili kutoa huduma kwa wananchi lakini kimepatiwa wafanyakazi wake kutoka zahanati “b” ambayo sasa zahanati hiyo haijitoshelezi wafanyakazi wake lakini pia zahanati “c” wafanyakazi wake ni wachache.

Mawazo yangu na fikra zangu ni katika kutazama upande mwingine wa shilingi ambapo kama serikali inatakiwa kuangalia muafaka wa wanaokuja kwenye tatizo hili yani upande wa kwanza wa shilingi lakini pia serikali inatakiwa kuangalia wale ambao tayari wapo kwenye tatizo hili yani upande wa pili wa shilingi, lakini pia kuangalia shinikizo la tatizo hili hapo baadae linapokuja kuwa kubwa zaidi nchini.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom