Kujitegemea mwenyewe

Kujitegemea mwenyewe

Hao Wazazi bado wana mawazo ya kizamani kuwa binti hawezi kuishi mwenyewe kabla hajaolewa ataonekana hana nidhamu. Na umri utakapokwenda sana akaamua kuzalia hapo nyumbani watamruhusu? au ndio atapokea kipigo?
na ndio wanachotakiwa wakisubirie hicho
 
wanao ila bado wako vyuoni huyo ndio first born na ameanza kazi kama mwaka na nusu sasa
 
Kama ananyimwa kutoka/kuchelewa nyumbani, na kama ananyimwa hata kwenda saluni....atampataje mme?? au hawataki aolewe (sababu za kiuchumi) labda....
Ila ukubwa wa huyo dada anaujenga mwenyewe...anawaachia wazazi wake wamuamulie uwezo wake wa kumudu maisha?? Nadhani yeye ndo anafanya wazazi wake wamwone bado mdogo!
 
Yani hii ndio situation inayonikumba kwa sasa, inachosha sana. Sijui hata nifanyeje.
 
Ushauri hapo unatakiwa kuzingatia dini na kabila la Mzazi
 
kwa kweli alitueleza mengi sana mpaka tulimuonea huruma mengine ya ndani sana mwenyewe hata akienda saloon hivi wanamuandama wanamwambia unatumia hela nyingi kujiremba wakati unaona mboga kwenye fridge zimepungua si bora utumie hiyo hela kununulia nyama watu wale
kama imefikia hatua anasimangwa namna hii noway asepe tu.

nyumbani ni kutamu wala huwezi lazimishwa kukaa hasa kwa mtoto wa kike,ila kwa story hii inaonekana wazazi wana maslahi binafsi na binti yao.
 
Habari za leo wanajamvi?

Jana jioni nimekutana na kioja mtaani kuna dada mmoja yuko single amerudi nyumbani saa 6 usiku (anakaa kwa wazazi) wakagoma kumfungulia geti (alikuwa na gari yake) na baadae baada ya kupiga honi sana mzee wake akatoka na kumwambia inabidi ufuate masharti ya nyumba yangu, nimesema simfungulii mtu akirudi zaidi ya saa 4 usiku kwa hiyo nenda huko huko ulikochelewa. Yule dada ni mfanyakazi wa benki kama cashier na anadai alichelewa kwa kuwa alishindwa kubalance hesabu na alikuwa na short kubwa sana hivyo alichanganikiwa na alisahau hata kuwajujulisha kwao.

Sisi tukamshauri ahame kwa baba yake akajitegemee lakini akadai baba yake hataki kumruhusu ahame mpaka atakapo olewa ndio aende kwa mmewe lakini sio kupanga wakati baba yake ana nyumba nzuri na kubwa hapa mjini

Naomba maoni yenu kwenye hili maana lilituacha njia panda

Je mtoto wa kike anapopata kazi inabidi ahame kwao au asubiri mpk atakapoolewa? (hapa naongelea wanaofanya kazi ndani ya mji mmoja na walipo wazazi) maoni wandugu
Duu aliolewa? Its 14 years hopefully ni mshangaz

Cc Nourhan
 
Back
Top Bottom