Kujitokeza kwa malalamiko mengi ya watanzania kudhalilishwa na apps za mikopo, ni ishara tosha watanzania 98% sio waaminifu kwenye kukopeshwa

Accumen Mo

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2022
Posts
18,036
Reaction score
39,882
Mnaendeleeja ndugu zangu watanzania,

Rejea kichwa cha uzi hapo juu, kwa masikitiko napenda kuwaambia huu ukweli , watanzania wengi sio waaminfu linapokuja suala la kukopeshwa .

Hizo apps zisingekuwa zinawadhalilisha kama mngekuwa mnalipa, kwanza mda wa marejesho mnakubali wenyewe ila baadae mnadai mnadhalilishwa. Ukweli mchungu hapa Tz ukimkopesha mtu lazima itakuja shida wakati wa kukulipa hata kama pesa anayo.

Siwezi kulaumu wale wanaoshikia watu kadi zao za bank wala wanadhalilisha watu, ikiwa walishafanya makubaliano ya awali mda uliopangwa kurejesha mkopo.

Ukija kwa sisi ndugu na marafiki wa karibu tunakopesha bila ya riba ila bado ni kimbembe mpaka kugombana, kwa dunia ya sasa haswa Tz ishu ya uaminifu ni lulu, sio rahisi kukutana na mtu muamifu iwe kweny pesa au mapenzi.

Mimi binafsi nimepoteza pesa na watu kibao kwa ujinga wao, moja ya kijinga jamaa alikopa pesa yangu pesa ndogo sana laki 1 ila alikuja kununua kiwanja cha mbele angu cha million 10 nikiwa nae beneti, lakini laki yangu hataki kunilipa. Alivyokuwa mpuuzi alikuja tena nimkopeshe nikamkumbusha deni la awali eti kasahau.

Tubadilike, sio kulalamika wao wana haki ya kuwadhalilisha.​
 
Na nimesikia data za wakopaji wa simu kama Songesha, Timiza na takataka kama hizi zimeongezwa kwenye Credit Bureau ya Tanzania.

Sasa hivi mtu unaweza kosa mkopo wa maana benki kisa ki-10,000/- unachogoma kulipa huko M-pesa.
 
Na nimesikia data za wakopaji wa simu kama Songesha, Timiza na takataka kama hizi zimeongezwa kwenye Credit Bureau ya Tanzania.

Sasa hivi mtu unaweza kosa mkopo wa maana benki kisa ki-10,000/- unachogoma kulipa huko M-pesa.
Watu sio waaminifu kabisa
 
TANZANIA NDIO NCHI PEKEE TASISI ZA KIFEDHA ZINAJIPANGIA RIBA KUBWA.WE UNADHANI KWA NINI KILA KAMPUNI ZINAKIMBILIA HAPA.

Mtoa mada unatatizo moja cha kwanza ujawai kuishi nchi za watu ndio maana unaona mapungufu.
wenzetu mikopo yao ina riba ndogo na unaweza kumudu ukilinganisha hapa.
subiri ujifunze kwa benk ya ABSA KUHUSU MKOPO WA GARI
 
Unekurupuka kutetea hao majambazi.

Mfano, unakopeshwa 78,000 ,unarudisha 120,000 tena ndani ya siku 5 mpaka 6. Ikifika siku ya 7 na zaidi, wanaanza kusambaza taarifa zako kuwa umewatapeli wakati mwanzoni mkopo ulikuwa ni wa siku 7 hata kama unawasilianao na kuomba wakuongezee sku 2 au 1.

Hao sio watu kabisa ni wanyonyaji wakubwa.

Nchi zenye serikali makini, haziwezi kulea huu upuuzi Ni katika nchi zenye mambo ya hovyo kama kupiga dili ya vibali vya sukari ndio upuuzi kama huu unashamiri.
 
Huku mitaani tunawakopesha bila ya riba ila hamlipi . Wee rafiki zako unakopesha kwa riba?
 
Mbona sisi jamaa zenu bila ya riba hata miezi 3 ila hamlipi bora mdhalilishwe.
 
Na nimesikia data za wakopaji wa simu kama Songesha, Timiza na takataka kama hizi zimeongezwa kwenye Credit Bureau ya Tanzania.

Sasa hivi mtu unaweza kosa mkopo wa maana benki kisa ki-10,000/- unachogoma kulipa huko M-pesa.
Upo sahihi. Nilirequest statement huko credit info mtu unajikuta kumbe uliwahi kukopa benki kupitia hizi songesha na nivushe.
Mpaka mikopo ya simu inawekwa kule.
 
Na nimesikia data za wakopaji wa simu kama Songesha, Timiza na takataka kama hizi zimeongezwa kwenye Credit Bureau ya Tanzania.

Sasa hivi mtu unaweza kosa mkopo wa maana benki kisa ki-10,000/- unachogoma kulipa huko M-pesa.
Mikopo hiyo kweli unawekwa CRI
 
Tubadilike, sio kulalamika wao wana haki ya kuwadhalilisha.
Haki ya kukudhalilisha hawana ila ni kweli wabongo ishu ya uaminifu ni 0.

Hizo App kuna vitu wanakosea wenyewe hadi mtu deni linakua kubwa na lisilolipika.
Kwenye matangazo yao wanasema utapewa mkopo siku 180, ila kwenye app ni siku 7 tu. Na ukishindwa siku hizo wanakulamba riba ya 11% ya deni lako.

Na mbaya zaidi zikiisha hizo siku 7 ya 8 au hiyo hiyo ya 7 tegemea kudhalilishwa. Sasa mtu ushampaka tope atakulipaje lazima aingie mitini tu.

Na shida niliyoiona kwa hao jamaa ni kua wanaajiri hovyo tu, vijana wengi kwenye hizo ofisi zao hawana utaalamu wowote wa hayo mambo. Wanapewa maelekezo ya kuchafua watu toka kwa boss wao mchina.

Na mbaya zaidi wanakopesha yeyote tu coz nadhani hawana wataalamu wa mifumo au nao ni janjajanja tu. Hata uwe na rekodi mbovu ya mikopo kwenye simu yako utakopeshwa tu.
 
Hii ni takwimu tosha watanzania wana hali ngumu kimaishaa πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ€“πŸ‘
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…