Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Mnaendeleeja ndugu zangu watanzania,
Rejea kichwa cha uzi hapo juu, kwa masikitiko napenda kuwaambia huu ukweli , watanzania wengi sio waaminfu linapokuja suala la kukopeshwa .
Hizo apps zisingekuwa zinawadhalilisha kama mngekuwa mnalipa, kwanza mda wa marejesho mnakubali wenyewe ila baadae mnadai mnadhalilishwa. Ukweli mchungu hapa Tz ukimkopesha mtu lazima itakuja shida wakati wa kukulipa hata kama pesa anayo.
Siwezi kulaumu wale wanaoshikia watu kadi zao za bank wala wanadhalilisha watu, ikiwa walishafanya makubaliano ya awali mda uliopangwa kurejesha mkopo.
Ukija kwa sisi ndugu na marafiki wa karibu tunakopesha bila ya riba ila bado ni kimbembe mpaka kugombana, kwa dunia ya sasa haswa Tz ishu ya uaminifu ni lulu, sio rahisi kukutana na mtu muamifu iwe kweny pesa au mapenzi.
Mimi binafsi nimepoteza pesa na watu kibao kwa ujinga wao, moja ya kijinga jamaa alikopa pesa yangu pesa ndogo sana laki 1 ila alikuja kununua kiwanja cha mbele angu cha million 10 nikiwa nae beneti, lakini laki yangu hataki kunilipa. Alivyokuwa mpuuzi alikuja tena nimkopeshe nikamkumbusha deni la awali eti kasahau.
Tubadilike, sio kulalamika wao wana haki ya kuwadhalilisha.