SoC02 Kujitolea kunalipa maradufu

SoC02 Kujitolea kunalipa maradufu

Stories of Change - 2022 Competition

Papaa Riziki

New Member
Joined
Sep 7, 2022
Posts
3
Reaction score
2
Kama Wahenga wetu walivyosema'Ndege anayetaka kutua kwenye bua la mtama ale sharti Kwanza atue kwenye mti wa pembeni ili aone vizuri bua lenye mtama mzuri'.

Kujitolea ni Hali ya kufanya shughuli Fulani bila kutanguliza malipo au maslahi binafsi.

Mwalimu mmoja wa shule moja ya Msingi aliishi katika mazingira yenye watoto na vijana wenye changamoto za umaskini,ulevi,wizi,ujinga na maradhi .Hii ilitokana na baadhi yao kuwa yatima na wazazi kukosa uwezo wa kuwapeleka shule.

Mwalimu pia alikuwa no muumini wa dhehebu Fulani pale alipoishi.Ndipo aliamua kuomba jengo mojawapo la dhehebu ili kwa muda wa ziada awe anakutana na hao watoto na vijana wenye mazingira magumu kuwatia moyo na kuwafundisha stadi za maisha pia kusoma na kuandika bila malipo yoyote..Alitumia kipato chake kidogo katika mshahara wake kuwapa chakula na mavazi.

Tendo Hilo liliwagusa wengi ikiwemo Serikali,watu binafsi,taasisi mbalimbali na mashirika yakiwemo World Vision na Right to Play ambao walianza pia kuchangia misaada.

Kupitia Mbunge baada ya kuwasilisha Hoja kuhusu yule mwalimu Ndipo Serikali ikaamua kuanzisha mpango uitwao MEMKWA yaani MPANGO WA ELIMU YA MSINGI KWA WALIOIKOSA.Walimu maalumu walianza kuandaliwa kupitia semina na madarasa yakaanza kujengwa kwa msaada wa Serikali na Wadau mbalimbali.Watoto nchi nzima waiokosa Elimu wakaanza kupata elimu bure.

Kupitia kujitolea yule mwalimu uhalifu ulipungua mitaani,umaskini,ujinga na maradhi vilipungua kwani wengi walikwenda shule kupata ujuzi na stadi za maisha wakajiajili na kuajiliwa.Mwalimu Nate akapata ufadhili wa kwenda kuongeza ujuzi ndani na nje ya nchi.Sasa mwalimu ni Afisa katika wizara ya TAMISEMI.

BY EZRON RIZIKI MBOGAMBI
 
Upvote 3
Back
Top Bottom