Watanzania salamu, ndipo nashika karamu, Naleta jambo muhimu, Fungua zenu fahamu, Umasikini Ni sumu, unaoleta magumu, kujituma ni silaha,na kazi iendelee.
Ukilala ni hasara, utaitwa ni fukara, omba omba inakera, kwa wengi unajichora, fanya kazi barabara, kipato kiwe imara, kujituma ni silaha na kazi iendelee.
Kama wewe ni kijana, Muda wako nii amana, Zingatia kazi Sana, Fanya mengi ya maana, Ujiwekee hazina, Uvutie kila Kona, Kujituma ni silaha, na kazi iendelee.
Uchumi wa digitali, utakufikisha mbali, piga konde yako hali, tengeneza zako mali, Furaha Kama asali,utaipata chakali, kujituma ni silaha, na kazi iendelee.
Bila pesa utasota,Marafiki hutopata,wapo wengi watapita,huku wamekula ndita,Jitume bila kusita,kuuzuia utata, kujituma ni silaha, na kazi iendelee.
Tambua nafasi yako, kuna watu nyuma yako, wasubiri lako cheko, wauone mwanya wako,kufuata nyayo zako,kuupokea upako, kujituma ni silaha, na kazi iendelee.
Sababu ya uharifu,Ni kipato Cha upofu, Fanya kazi bila hofu, Maisha yawe nadhifu, Nguvu kazi Kama bafu, linasitiri machafu, kujituma ni silaha, na kazi iendelee.
Jiulize swali hili, Kisha waza kwa akili, unaona Nini mbali, kuandaa zako Mali, moja na moja Ni mbili, usife moyo awali, kujituma ni silaha, na kazi iendelee.
Naweka msisitizo, tujitume kwa uwezo, Tutatue matatizo, tusiumie kwa tozo, Tuweke kando chukizo, Tuwajibike kwa mkazo, Kujituma ni silaha, na kazi iendelee.
Alana Ni langu jina, Popote napatikana, Nitafute kila Kona, nikupe yenye maana, ujipatie hazina, ilo bora na kunona, kujituma ni silaha, na kazi iendelee.