Kujiunga na Kijiji kisha Kupewa Shamba!!

Kujiunga na Kijiji kisha Kupewa Shamba!!

Shakir

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
1,627
Reaction score
1,926
Wadau,

Nilipata kusikia kua kuna vijiji unaweza kuomba uanachama wa kijiji ukawa na wewe ni mwanakijiji mwenzao kisha ukiomba mashamba wanakupa (yoteyote).

Hii nimeisikia kua kuna taratibu za kuomba huo uanachama wa kijiji kwa kulipia gharama mbalimbali za vikao vya kukujadili, posho za wajumbe e.t.c.

Wakati wa kusuburi hao wanakijiji kukujadili inatakiwa uwe unatembelea mara kwa mara kijijini kupiga nao story za hapa na pale, ikiwezekana ukiwakuta hata maskani wanacheza bao au kupiga story nawqe unajiunga nao, na kama ni kwenye vilabu basi unazungusha nao raundi kama kawaida.

Nimeambiwa kua kwa mtaji huu unaweza ukapewa hata Hekari 50 - 100 kwa gharama labda isiyozidi 1.5Million kwa jumla. Na maeneo ya Mkoa wa Pwani ndani ndani huko (tuseme labda Kisarawe, Chole Samvula, Mzenga, e.t.c) ndio mambo haya yapo.

Kuna mdau yoyote mwenye idea na hii kitu?
Najua kuna wadau wangu wa kilimo hapa wako deep kwenye hizi issue.
 
Unaandika barua ya kuomba kuwa mwanakijiji, then watakujadili. UKikubaliwa utapewa eneo la kujenga kijijini pamoja na shamba la bure hekari 5 tu. Ukiamua kuama na kuishi mbali na kijiji hicho, itakupasa kuchangia michango yote inayohusu maendeleo ya kijiji hicho.

Kuhusu kupata ekari 50 na kuaendelea, hii itakulazimu uingie kijijini kama mwekezaji napo kuna taratibu zake.
 
Kwa kutumia gear hiyo nyanda za juu kusini magharibi utafanikiwa.karibu
 
Ahsante Mkuu kwa taarifa, heka 5 pia si haba.
Sasa mfano Kijiji gani wana huo utaratibu?
 
Kwa kutumia gear hiyo nyanda za juu kusini magharibi utafanikiwa.karibu
Mkuu nimeambiwa kwa vijiji vya mkoa wa pwani hiyo kitu ipo. Kwa sisi tunaoishi Dar, siku moja moja labda wikiend kwenda kisarawe kujichanganya na wenyeji na kupiga nao story sio issue kubwa sana, tofauti na kufunga safari hadi huko nyanda za juu kusini magharibi.
 
mkuu nimeambiwa kwa vijiji vya mkoa wa pwani hiyo kitu ipo. Kwa sisi tunaoishi dar, siku moja moja labda wikiend kwenda kisarawe kujichanganya na wenyeji na kupiga nao story sio issue kubwa sana, tofauti na kufunga safari hadi huko nyanda za juu kusini magharibi.
iko hivi...kuna wadada, tena wanatoka kenya wanamiliki ma hekta ya ardhi sumbawanga na namtumbo,,sasa kama una uwezo changamka....usije ungana na watakao lalama baadae.
 
Nimeipenda hii; mi naenda zangu Simiyu huko nikajichukulie eneo la kutosha
 
Inawezekana kabisa! mimi nilishaenda kijiji karibu na maneromango jina nmesahau labda nikisoma document baadae walinipokea vizuri! ekari kumi za kuanzia
 
Singida unapewa aridhi na mifugo ya kuanzia maisha

mfn ndama wawili au mbuz wanne
 
Mkuu nimeambiwa kwa vijiji vya mkoa wa pwani hiyo kitu ipo. Kwa sisi tunaoishi Dar, siku moja moja labda wikiend kwenda kisarawe kujichanganya na wenyeji na kupiga nao story sio issue kubwa sana, tofauti na kufunga safari hadi huko nyanda za juu kusini magharibi.

hahahaa, kaka angalia kauli hiyo, watu wanavuka bahari wewe unaogopa kuoanda basi masaa12!!!!
 
Nimeipenda hii; mi naenda zangu Simiyu huko nikajichukulie eneo la kutosha

Mkuu hata miye naona hii imekaa vizuri, ni kujaribu ku-practice tu popote pale, kwani hao walioko vijijini wana maeneo makubwa waliyapataje? Ngoja tujaribu bwn unaweza jikuta umemiliki maeneo ya kufa mtu.
 
Sema sasa Mkuu ukiingia kwenye vijiwe vya mataputapu huko kijijini na wewe inabidi ugonge nao kimtindo ili wakuone mwenzao.
 
Back
Top Bottom