Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
KUJIUNGA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NI HIARI, KWANINI WALIMU WANALAZIMISHWA KUJIUNGA VYAMA VIWILI VIWILI
"Je, ni faida gani ambayo wafanyakazi wanapata kupitia uwekezaji wa fedha wanazokatwa na vyama vya wafanyakazi"? - Mhe. Neema Gelard Mwandabila, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe
"Faida ambayo wafanyakazi wanapata kupitia uwekezaji wa fedha wanazokatwa na vyama vya wafanyakazi ni pamoja na vyama vya wafanyakazi kusuluhisha migogoro ya kikazi kwa niaba ya wanachama wake, kutoa huduma kwa wanachama kama vile ya utetezi katika Mahakama ya kazi na kutoa Elimu kuhusu Sera na Sheria za kazi kwaajili ya maslahi mapana ya wafanyakazi.
Pia, huzitumia kutekeleza majukumu ya vyama yaliyowekwa kikatiba na kisheria yanatokana na uwepo wa vyama mahali pa kazi. Vipo baadhi ya vyama vya wafanyakazi ambavyo hutumia ada za uanachama kujenga majengo kwaajili ya matumizi ya Ofisi ya vyama, kuwapangisha watu mbalimbali na kutoa huduma kwa wanachama wao. Fedha hutumika kuongeza bajeti za vyama vya wafanyakazi ili waweze kutekeleza majukumu ya kikatiba na kisheria kikamilifu" - Mhe. Ummy Hamis Nderiananga, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
"Ada za wafanyakazi zinatumika kwenye uwekezaji kama kujenga majengo; Natamani kufahamu ni lini Serikali itakuja na Sheria ambayo inampa haki mwanachama kuweza kupata gawio kwa fedha zinazopatikana kwa uwekezaji huu! - Mhe. Neema Gelard Mwandabila, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Songwe
"Kumekuwa na malalamiko mengi ya walimu kulazimishwa kuingia kwenye vyama 2 vya wafanyakazi, Ni lini kauli ya Serikali kuhakikisha kwamba kujiunga na uanachama wa vyama vya wafanyakazi ni hiari ili kusiwepo na kulazimishana kuingia kwenye vyama viwili viwili vya wafanyakazi? - Mhe. Neema Gelard Mwandabila, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Songwe
"Sheria ipo ambayo inaviruhusu vyama vya wafanyakazi na zipo kanuni ambazo zinawaongoza katika vyama vyao kwa misingi ya katiba walizojiwekea. Nichukue kama maoni katika eneo hili, nitaonana naye baadaye ili tuweze kuzungumza zaidi kuona nini alimaanisha" - Mhe. Ummy Hamis Nderiananga
"Vyama vya wafanyakazi ni vya kihiari lakini Katiba zao ndiyo zinawabana pengine ujiunge au ukijiunga utanufaika na nini/kipi. Siyo lazima kwa kulazimishwa ujiunge kwenye vyama vya wafanyakazi, hapana!" - Mhe. Ummy Hamis Nderiananga