Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
KUJIVUA GAMBA KWA NYOKA HAKUMFANYI ASIWE NYOKA. MSALITI NI MSALITI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
1. Usidanganywe na Werevu wake. Nyoka ni nyoka.
2. Nyoka anapojivua gamba ili aonekane mpya. Kabadilika ni mbinu ya kimedani. Sio kwaajili yako. Ni kwaajili yake mwenyewe.
3. Kimahusiano hiyo ni hadaa. Anakudanganya.
4. Kikawaida msaliti hasaliti mara moja ukimpa nafasi mbili au tatu.
Wasaliti akikusaliti ya Kwanza ukampa nafasi ya pili atakusaliti pia.
5. Sisi Watibeli tunaongozwa na kanuni isemayo, When someone trust and believe you never depend on second chance. Kwamba ukiaminiwa na mtu usitegemee nafasi ya pili pale utakapoharibu uaminifu huo.
6. Hatuzungumzii ukamilifu. Tunafahamu binadamu hajakamilika. Lakini kanuni nyingine ya kitibeli inasema, "Tunasamehe Makosa lakini sio uhalifu/uovu"
7. Binadamu hajakamilika hivyo inategemewa kufanya Makosa. Lakini binadamu hakuumbwa kufanya uhalifu, uovu.
8. Makosa ni Yale mambo unayoyafanya bila kukusudia, bila kuwa na utambuzi. Bila kujua au zile errors za kibinadamu.
Lakini Dhambi/uhalifu ni mambo unayoyafanya kwa dhamiri, ukikusudia na kujua hili ni kosa, na bado unafanya.
9. Nyoka hufanya uhalifu/uovu kwa makusudi kabisa. Ndio maana Sisi watibeli hatutoagi nafasi ya pili.
10. Mtu unamtendea Wema, vizuri tuu. Unakuwa kwake mwema. Leo anakulipa mabaya kimakusudi. Alafu baadaye anakuambia ni shetani.
11. Vijana na mabinti, wakubwa kwa wadogo. Wapo baadhi yenu mmekuwa mkiteswa na kuteseka, kuumizwa kisa Wema wenu. Wengine mmekuwa mkinipigia simu na kunitukia jumbe kwenye mails, JF, FB, WhatsApp, na normal SMS, kwa mambo yaliyowatokea.
12. Msimamo na falsafa za watibeli ni zilezile hazijabadilika. Nyoka ukishamtambua hutakiwi kumsamehe, hatakiwi kuwa karibu yako.
13. Wapo Wanawake visa vyao vinaumiza Sana. Wameteswa na waume zao Sana. Nilipobahatika kukutana na Waume zao ili kubalance mzani. Wanaume walionekana wakaidi, wasiojali, wenye dharau, baada ya kutengana muda ukapita. Mwanaume anajirudisha, ananipigia simu kuwa sasa yupo tayari kuweka mambo Sawa na familia yake.
14. Wakati huo mwanamke ameshaendelea na Maisha yake, na yupo mbioni kuolewa. Nikamwambia mwanaume. Wewe ni nyoka. Na kikawaida nyoka anatakiwa kupondwa kichwa na sio vinginevyo. Akaniambia amebadilika. Nikamwambia nyoka kujichubua na kujitoa gamba haimfanyi awe Samaki. Nyoka ni nyoka.
15. Akaondoka na hasira, akawa anambembeleza Yule mwanamke. Yule mwanamke akawa ananipigia kuomba ushauri. Nikamuuliza ushauri UPI. Kama mtu alikuacha kwa namna ile? Hakuwa amelewa na nisingeruhusu kuwa na kikao na mtu aliyelewa. Alikuwa mzima. Aliongea akimaanisha.
16. Mwanamke akasema acha ampe nafasi ya mwisho. Kwani wanawatoto wawili. Nikamwambia kikawaida nyoka akikung'ata alafu akaona hakukung'ata vizuri round ya pili atakupiga katafunua kubwa lao. Akasema atakuwa makini. Hiyo ilikuwa mwisho wa mwaka Jana.
17. Juzi hapa, Yule dada ananipigia simu Analia kama Mwehu.
Kumbe na mkopo alimchukulia, kwani ni Muuguzi kwenye moja ya hospitali hapa jijini Dar es salaam.
18. Mkopo umeenda kwa mwanamke mwingine. Yaani unamchukulia mkopo mwanaume wako afanyie biashara, alafu hiyo biashara mwanaume wako kamfungulia mchepuko wake. Dadeki!
19. Nikamwambia asiniambie ujinga wake. Akawa Analia akiniomba msamaha kwamba hakunisikiliza. Nikamwambia ajiombe mwenyewe kwa kujikosea.
20. Wameachana kwa aibu na maumivu zaidi. Huku mwanaume akionekana mshindi kwani kaondoka na faida zaidi kuliko hasara.
21. Huo ni mfano katika mahusiano ya wanandoa au watu wanaoishi kama mume na mke.
22. Kimedani, katika Siasa au kijeshi. Hawa kidogo wanajua nini chakufanya.
Wanajua msaliti hapewagi nafasi.
23. Na kisiasa au kijeshi wasaliti huwaga wanauawa bila mijdala mingi na bila kujali kuna Sheria au hakuna. Kuna serikali au hakuna serikali.
24. Hamuwezi kukaa na wenzako mnajadili Jambo. Mmepatana kabisa. Na kama kulikuwa na hoja hukutoa. Ulikaa kimya. Alafu baada ya kikao unaleta usaliti. Watakula kichwa.
Haya labda ulizungumza, lakini kwenye vikao kuna kauli ya wengi wape.
Mpo wawili mnaopinga hoja Fulani. Lakini watano wamekubali. Basi wengi wanapewa. Ndivyo mambo yalivyo kwenye familia, taasisi, vyama na mambo ya kijumuiya.
25. Nyoka akijivua gamba haimaanishi anageuka Samaki. Hapana. Nyoka ni Nyoka.
26. Kingine sio Kila kosa ni Usaliti. Hapana. Makosa mengine ni kutokuelewana.
27. Mfano Mkeo hajawahi kukusaliti kingono. Ila mmepishana kauli yeye akaenda nyumbani labda kuepusha shari ya kupigana, au mumeo akaondoka akahama nyumba kwa muda lakini sio makosa ya usaliti wa mapenzi. Huo sio unyoka.
28. Unyoka ni nini?
29. Unyoka ni hali ya kuwa adui yako lakini anapita nyuma ya mgongo wako. Anajifanya MTU mzuri, anakuchekea, mnapatana vizuri kumbe anapita nyuma ya mgongo wako.
30. Anaungana na adui zako. Anakuhujumu. Anampa nguvu adui yako. Huyo ni Nyoka.
31. Nyoka anatembeza sumu kwa watu ili uonekane mbaya. Anachafua jina lako. Lakini akiwa mbele yako anajifanya mwema kwako na hajawahi kukuchana. Huyo ni nyoka.
32. Anatoa siri zako, madhaifu yako kwa watu. Huyo ni nyoka. Na kwa Sisi Watibeli. Tunajua nini chakufanya. Na hatunaga uvumilivu hata kidogo.
Acha nipumzika sasa.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam