Kujua hesabu utoto raha sana, cheki hii

Daviie

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2016
Posts
1,294
Reaction score
1,480
Nimekuta madogo watatu wanagawana maandazi. Wamenunua maandazi mawili sasa kila mmoja anataka achukue moja halafu atakayekosa wamgawie, kilichonichekesha ni dogo mmoja kajiongeza fasta kawabia haya chukueni mnikatie nusu nusu. Madogo waliochukua maandazi wamefurahi wakajiona wajanja sana halafu wakamkatia mwenzao nusu nusu tena kwa tabasamu usoni wakifikiri wao ndo wamefaidi kumbe wamejipunja bila kujua.
Kweli kujua hesabu raha sana. Hebu tukumbushe wewe utotoni ulitumia mbinu gani kuwapunja wenzako vitu mlivyopaswa kugawana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nilikuwa nikitumwa naomba nyongeza, nikipewa nyongeza nagonga kwanza na nikipeleka nilichotumwa mgao uko pale pale[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

"[ᴬ ᵍᵒᵒᵈ ᵖˡᵃⁿ ᵛⁱᵒˡᵉⁿᵗˡʸ ᵉˣᵉᶜᵘᵗᵉᵈ ⁿᵒʷ ⁱˢ ᵇᵉᵗᵗᵉʳ ᵗʰᵃⁿ ᵃ ᵖᵉʳᶠᵉᶜᵗ ᵖˡᵃⁿ ᵉˣᵉᶜᵘᵗᵉᵈ ⁿᵉˣᵗ ʷᵉᵉᵏ"
 
Namuombea Uyo dogo asiingie kwenye siasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenikumbusha mbali[emoji23]
Nilikuwa natumwa mbali kashata za Nazi.
Za Tzs100/= zilikuwa 10.
Halafu napewa kakashata kamoja tuu.[emoji17][emoji17][emoji17]

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Ulitaka upewe zote?

Mimi nakumbuka niliwahi kuokota tsh 100 (noti) nikaishia kupewa kitawa (ndizi zilizochanganywa na maziwa).
Nikikumbuka najiona nilikua mjinga sana kurudisha ile pesa.
 
Hahaha we noma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Ulitaka upewe zote?

Mimi nakumbuka niliwahi kuokota tsh 100 (noti) nikaishia kupewa kitawa (ndizi zilizochanganywa na maziwa).
Nikikumbuka najiona nilikua mjinga sana kurudisha ile pesa.
Mmmh sh mia ya noti ??? Mkuu utakuwa umekuwa mhenga sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…