Askofu na Mbunge wa Kawe Bishop, Dr Josephat Gwajima aliwahi kusema, namnukuu, "Kama hujui ulipotoka unaweza kuhisi kwa ulipo sasa umefanikiwa kumbe hapana ila unarudia makosa yako yale-yale huku ukidhani ni maendeleo"
HII INA-MAANA...
Toka nimekufahamu Kocha Makirita Amani (Miaka takribani sita sasa) na ulipo leo hii, Kiuandishi, Elimu, Maisha nk, bila shaka kuna hatua kubwa sana ambazo umepiga mpaka siku ya leo, na binafsi ninaamini kabisa kuwa kama utashidwa kuyatimiza maono yako basi utakuwa ni uzembe wako mwenyewe, maana kwa ulipo toka, ulipo sasa na unapoelekea ni ushahidi tosha kuwa kuna nguvu kubwa inakusukuma kwenda kutimiza maono yako.
LABDA....
Jua hili kabisa, kwamba tupo nyuma yako weeeengi sana tunaotiwa moyo na kuhamasishwa sana na-mafundisho yako kila wakati. Usitishwe kabisa na akina Yuda ambao wanasimama na kukupinga au kukuvunja moyo jua ni wivu tu, wewe songa mbele.
ILA....
Hakikisha siku umekaa kwenye kiti cha u-rais 2040 hakikisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iwe yangu (Mean uniteue)
Hapibezidei kwako Kocha,
Natanguliza shukrani,
Deus M.Ndololo