Kujuana kwa itikadi za CCM, undungu na Mazoea kunavyozorotesha uwajibikaji Zanzibar

Kujuana kwa itikadi za CCM, undungu na Mazoea kunavyozorotesha uwajibikaji Zanzibar

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,293
Mada inahusika.

Kwa miaka mingi ndani ya Serikali ya Zanzibar kumekuwa na mazoea ya kuchaguliwa kwa itikadi, kujuana na undugu.

Yaliyopita ni mengi, lakini kwa muktadha wa mada hii tuangalie hii miaka mitano kutoka 2015 - 2020.

Ikumbukwe Zanzibar inahitaji kuponywa majeraha mbali mbali ya ubaguzi na ndio maana kukawepo Serikali ya kitaifa walau kupunguza mianya hiyo. Aidha wasomaji wakumbuke kwamba kwa miaka hii mitano Serikali ya Umoja wa Kitaifa haipo na mambo yamezidi kuwa mabaya. Hebu fikiria uhalisia ufuatao.

i. Uajiri kuegemea milengo ya kisiasa ambapo kwa sasa kuwa mwana CCM ndio unapewa kipaumbele. Hata kama uwezo ni mdogo. Sio mara moja wala mbili wahusika wamekuwa wakikanusha lakini ukweli huu upo na hutumika taasisi inayoitwa GSO kukamilisha hayo.
Mifano ya wazi ni kuwepo taarifa za nafasi za baadhi ya waajiriwa kwa upande wa Pemba ambapo kunaaminika kuwa na wapinzani hupelekwa wana CCM kutoka Unguja kujaza nafasi hizo hasa kwenye Vikosi na nafasi za Muungano.

ii. Utendaji kazi maofisini kwenda kwa mazoea kwa kujuana. Huko maofisini ni deko kwenda mbele. wateule wengi hawana uwezo wa kufanya kazi na hupandishwa vyeo kwa kujuana kwa milengo ya kisiasa au undugu. Hatimaye ufanisi unapwaya na malalamiko hayaishi. Watu wenye uwezo wanawekwa pembeni kwa sababu za kisiasa.

iii. Kulindana kwa milengo ya kivyama. Hili ni tatizo sugu, Baadhi ya watendaji na viongozi wametopea kwenye rushwa na ufisadi. Zanzibar ni ndogo na taarifa zinaenea kwa haraka. Kuna baadhi ya viongozi wakubwa serikalini na mawizarani wanakula rushwa kupitia miradi mbali mbali na wanapata kinga. Miradi mikubwa inayotajwa kwa sasa ni ujenzi wa Kiwanja cha kufurahishia watoto, miradi ya ujenzi wa nyumba za ZSSF kule mbweni na kisonge. Aidha kuna ununuzi wa Meli ya MV Mapinduzi II ambayo viongozi wakubwa wamehusishwa nayo.
Licha ya kujulikana taarifa hizo, wahusika wanalindwa na Mamlaka zao za uteuzi kwa kujuana.

Pia kuna mifano ya watu kutowajibishwa kwenye kazi, kupendeleana kwa kupatiwa nafasi za masaomo, fursa za ushiriki na mafunzo n.k. Kuna watu ambao wangestahiki kupata fursa wanaCHUPWA KWA MAKUSUDI BILA KUTOFUATWA TARATIBU NA KUPEWA WENGINE KWA KUJUANA NA ITIKADI.

NINI KIFANYIKE?

Zanzibar kunahitaji mabadiliko ya dhati na utashi wenye uthubutu. Kunahitajika viongozi imara na jasiri kusimamia nidhamu ya kazi na kuondowa muhali. Hili la kuondowa muhali ni kubwa sana. Kuna watu wamependelewa sana na kufaidi fursa mbali mbali ambazo sio stahili yao.

Kunahitaji sera mbadala na uthubutu wa kuleta mageuzi ya kiutendaji serikalini. Kunahitajika "Total shift" ya utendaji na "Restructuring" ya Nguvu ili kubadilisha utamaduni mbovu iuliolelewa kwa miaka mingi ya Utawala wa CCM.

Utaalamu na ufanisi wa kazi upewe kipaumbele. Kwenye sekta zote hasa za Afya, elimu, mashirika ya kuingiza mapato na MIRADI MKAKATI.

Kishada.
 
Back
Top Bottom