Kujuzwa au kujuliswa?

Globu

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Posts
8,659
Reaction score
2,227
Habari zenu Wakuu, naomba kujua neno sahihi katika matumizi ya lugha ya Kiswahili. Jee ni kujuza, kujuzwa au ni kujulisha au kujulishwa? Nawasilisha.
 
Nasubiri maoni yenu wakuu. Samahani Heading isomeke KUJULISHWA.
 
Wataalamu wa lugha mpooo!!! Jumapili njema.
 
Nionavyo mie, kujuza ni mnyumbuliko wa nomino ujuzi. Sasa unapompatia mtu ujuzi unakuwa unatumia tendo la kujuza...Kwa maana hii, anayetenda huwa
anajuza na anayetendewa yaani kupewa huo ujuzi..yeye huwa anajuzwa.

Kujulisha ama kujulishwa...ni hali ya kutoa ama kupokea taarifa...
 
Yapo maneno ambayo ni sahihi katika mifumo yote miwili, ila matumizi yake hutofautiana kulingana na watu wa maeneo. Kwa mfano:

1. Funza/Fundisha [Funzwa/Fundishwa]
2. Juza/Julisha [Juzwa/Julishwa]

Juu ya hivyo, nilimsikia Profesa mmoja wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisisitiza kwamba licha ya kuwepo maneno ambayo yanakubalika kwa mifumo yote miwili, neno pagawa hutakiwa kubadilishwa kuwa kupagaza na sio pagawisha kama baadhi ya watu wanavyotumia

Maneno mengine ambayo ni sahihi kimfumo lakini mfumo utakaotumiwa utategemea eneo la nchi uliopo ni pamoja na:

1. Ua
--> Uliwa [Ukanda wa Pwani na Zanzibar]
--> Uawa [Tanzania Bara]

2. Fia
--> Filiwa [Ukanda wa Pwani na Zanzibar]
--> Fiwa [Tanzania Bara]
 

Kitendo cha kutendea na kutendewa [mfano: somesha/someshwa, lisha/lishwa,] daima hutokana na kitendo cha kutenda [mfano: soma, kula (la),] na sio nomino.

Kwa hiyo juza haiwezi kuwa imetokana na nomino, badala yake imetokana na kitendo jua.

Ukiangalia pia matumizi ya neno "kujuza" katika fasihi za zamani, utagundua pia halitumiwi kueleza ujuzi/ustadi.

Mfano: Jirani alitujuza kuwa atasafiri siku inayofuata
 
Gaijin yawezekana ukawa uko sahihi kabisa. Asante
 
Last edited by a moderator:

Nakubaliana na wewe. Ila kuna tabia siku hizi, utasikia mtu au mtangazaji wa redio au TV, anasema 'hebu nijuze' au 'tutakujuza kinachoendelea'. Wakati hii ni taarifa sio ujuzi. Jee huoni kama tunatumia maneno ambayo sio mahala pake. Ufafanuzi Mkuu.
 
Nakubaliana na wewe. Ila kuna tabia siku hizi, utasikia mtu au mtangazaji wa redio au TV, anasema 'hebu nijuze' au 'tutakujuza kinachoendelea'. Wakati hii ni taarifa sio ujuzi. Jee huoni kama tunatumia maneno ambayo sio mahala pake. Ufafanuzi Mkuu.

Kwa mujibu wa kamusi ya Madan iliyochapishwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1939 na Oxford University Press, neno juza linatokana na neno jua kama nitakavyokuanishia hapa chini.

Kwa hiyo, hiyo nadharia ya kuwa neno hilo limeanza kutumika kwa maana sawa na [kujulisha] katika siku za karibuni si sahihi. Mimi binafsi matumizi ya [kujuza] kama [kujulisha] nimekuwa nikiyasikia sana kwa Bibi yangu ambaeangelikuwa hai hivi sasa angelikuwa na umri wa zaidi ya miaka 100. Hivyo si mtindo mpya wala halitumiki kimakosa. Ni sahihi kabisa


Kwa hiyo sio tu kuwa Juza ni sahihi, lakini pia unaweza kutumia Juvya au Juvisha ukipenda.

*Pia angalia matumizi ya Juliwa, Julika na Julikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…