Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nionavyo mie, kujuza ni mnyumbuliko wa nomino ujuzi. Sasa unapompatia mtu ujuzi unakuwa unatumia tendo la kujuza...Kwa maana hii, anayetenda huwa
anajuza na anayetendewa yaani kupewa huo ujuzi..yeye huwa anajuzwa.
Kujulisha ama kujulishwa...ni hali ya kutoa ama kupokea taarifa...
Gaijin yawezekana ukawa uko sahihi kabisa. AsanteKitendo cha kutendea na kutendewa [mfano: somesha/someshwa, lisha/lishwa,] daima hutokana na kitendo cha kutenda [mfano: soma, kula (la),] na sio nomino.
Kwa hiyo juza haiwezi kuwa imetokana na nomino, badala yake imetokana na kitendo jua.
Ukiangalia pia matumizi ya neno "kujuza" katika fasihi za zamani, utagundua pia halitumiwi kueleza ujuzi/ustadi.
Mfano: Jirani alitujuza kuwa atasafiri siku inayofuata
Nionavyo mie, kujuza ni mnyumbuliko wa nomino ujuzi. Sasa unapompatia mtu ujuzi unakuwa unatumia tendo la kujuza...Kwa maana hii, anayetenda huwa
anajuza na anayetendewa yaani kupewa huo ujuzi..yeye huwa anajuzwa.
Kujulisha ama kujulishwa...ni hali ya kutoa ama kupokea taarifa...
Nakubaliana na wewe. Ila kuna tabia siku hizi, utasikia mtu au mtangazaji wa redio au TV, anasema 'hebu nijuze' au 'tutakujuza kinachoendelea'. Wakati hii ni taarifa sio ujuzi. Jee huoni kama tunatumia maneno ambayo sio mahala pake. Ufafanuzi Mkuu.
Jua, v. know, know about, understand, be acquainted with. Ps. Juliwa. St and Pot. Julika and Julikana, be known, be knowable, be intelligible. Cs. Julisha (rarely Juza), cause to know, make known, inform. Also Juvya, and Juvisha (sometimes meaning 'make impertinent, provoke to or teach impertinece)