Kula chakula chepesi nyakati za usiku,lala kwa wakati na jifunze kulala kifudifudi.Hamna cha mapepo wala majini.Hizi habari za kuaminishwa kuhusu mapepo zimewafunga watu wengi sana fikra
Kwa vile hujawahi kukumbana na mambo hayo ndo maana unaweza kuandika kwa dharau hivi. Mapepo yapo na yanawatesa watu saana tu. Wengine mpaka wanaingiliwa nayo bila ridhaa yao. Wanawake hawataki hata kuolewa na kama ameolewa hamtaki kabisa mume wake, wanaume hawana haja na wanawake na wale wanaojitutumua na kuendelea kukaa na wake zao hao wanawake wanapatwa na ajali za ghafla na kututoka.
Weye acha kudharau makitu hayo. Sipo hapa kuandika ili kuwaogofisha watu ila, kwa yule yanampata namwambia njia pekee ni maombi na kinga pekee ni Jina lipitalo majina yoote; Jina la YESU KRISTO WA NAZARETH tuuuu.
Sintamtetea huyo Yesu kwani anajidhihirisha yeye mwenyewe kwa kila amwaminiye. Mathayo 11 : 28 Yesu anasema; Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha.
Huyu ndiye nabii pekee aliyeweza kuwaambia wanadamu maneno kama hayo.