Kukabwa usiku na kushindwa kupumua vizuri usiku ukiwa umelala

Kula chakula chepesi nyakati za usiku,lala kwa wakati na jifunze kulala kifudifudi.Hamna cha mapepo wala majini.Hizi habari za kuaminishwa kuhusu mapepo zimewafunga watu wengi sana fikra

Kwa vile hujawahi kukumbana na mambo hayo ndo maana unaweza kuandika kwa dharau hivi. Mapepo yapo na yanawatesa watu saana tu. Wengine mpaka wanaingiliwa nayo bila ridhaa yao. Wanawake hawataki hata kuolewa na kama ameolewa hamtaki kabisa mume wake, wanaume hawana haja na wanawake na wale wanaojitutumua na kuendelea kukaa na wake zao hao wanawake wanapatwa na ajali za ghafla na kututoka.
Weye acha kudharau makitu hayo. Sipo hapa kuandika ili kuwaogofisha watu ila, kwa yule yanampata namwambia njia pekee ni maombi na kinga pekee ni Jina lipitalo majina yoote; Jina la YESU KRISTO WA NAZARETH tuuuu.
Sintamtetea huyo Yesu kwani anajidhihirisha yeye mwenyewe kwa kila amwaminiye. Mathayo 11 : 28 Yesu anasema; Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha.
Huyu ndiye nabii pekee aliyeweza kuwaambia wanadamu maneno kama hayo.
 

kwa msaada zaidi ni pm.
 
Mimi ni mhanga wa hii hali zaidi ya miaka 10 sasa! Ila very amazing huwa ikinitokea tu najikakamua kuliita jina kuu liyaptayo yote; "KWA JINA LA YESU" ndio kiboko yake, hakuna cha pua ya nguruwe mbavu wala kulala kifudifudi!
 
pole sana ndug...hii huwatokea wengi..dawa ni kidogo sana AMINI NA UTII!! YESU KRISTO WA NAZARETI NDIYO DAWA.Wewe ukilala sema Yesu naomba ulinzi wako na utalala kwa amani kwani anasema katika Yer 33:3 NIITE NAMI NITAKUITIKIA NAMI NITAKUONYESHA MAMBO MAKUBWA NA MAGUMU USIYOYAJUA..Hakuna anayemwita akateseka kwa mapepo wala majinamizi...
 
duh mi naona watu wa yesu wanavutia kwao tu, upande wa mudy mbona kimya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…