Kukamatwa Juzi kwa Kato Rasta Muuaji wa Afande Muna Kawe ni jibu tosha kuwa huwezi Kuikimbia popote pale Jamhuri kama ikikutaka

Furaha yangu ni kwamba Muna hatofufuka kamwe.

Askari wa Jeshi la Wananchi wanapaswa kutumia akili sana na busara linapokuja suala la muingiliano na raia.

Ni ushamba mwanajeshi kutaka kila anakopita aogopwe badala ya kuheshimiwa, fanye kazi zenu heshimuni Wananchi msiwaonee kisa mna uniforms. Kila kitu hupita haya yuko wapi Afande Muna? anaacha familia bila sababu ya msingi ubabe usio na maana na kutaka sifa za kijinga.

Kwanza nashindwa kuamini kama alikuwa Afisa wa Jeshi kweli maana kwa kisa kilichosimuliwa anafanana na Private wa Jeshi aliyeanza kazi jana tena yule mshamba mshamba.
 
Hili nakubaliana na wewe kabisa
 
Kuna mwamba ana kesi nzito lkn huu ni mwaka hajakamatwa anaishi kiculture sana huyo jamaa.. sijui huyo Rasta alikuwa haishi kiculture
Hao ni experienced criminals but at last watadakwa tu. Utakuwa unafanya kosa kubwa kumlinganisha Kato na wahalifu kama akina Ayman Zawahir, Usama bin Laden, etc. ambao hata hivyo mwisho walidakwa au kuuwawa sembuse Kato asiye na ufahamu wa lolote la maana.
 
Alifia angani huyu mwamba alivyojump.
 
Hivi kweli mhalifu wa level ya kuteka ndege na Kato mwedesha bajaji Kawe wapi na wapi! Mbona tunafananisha visivyofananishika?
 
Hapo kwenye uvuvi nenda katika visiwa vidogo vidogo vilivyopo ziwani hasa huko Kanda ya Ziwa. Huko hakuna minara ya simu. Endelea kuvuna majarife/ makokoro bila wasiwasi.
Kuna kisiwa kinaitwa maisome kingine kinaitwa izumacheli viko kanda ya ziwa kwenye ziwa victoria sengerema ndani ndani huko aisee nina uhakika ukiweza kuingia kwenye visiwa hivyo ukatulia hawakupati aisee kwanza hakuna kituo cha polisi wa network.
 
Hapa unazungumzia Ma mbele huko siyo bongo

Kwa maana hiyo jamaa kupita mikoa yote hiyo alitembea kwa miguu?
Mbishi uswazi acha ubishi kama jina lako lilivyo.

Serikali ina mkono mrefu sana Ndugu yangu cha msingi ni kuomba tu Mungu yasikukute.

Hujiulizi yule Mjeshi aliyeuliwa nnje ya nchi South Africa baada ya kupishana na Mkuu wa nchi jirani?

Je yule aliyefanya mauaji Zanzibar afu wakaja Wataalamu toka USA wakachukua picha yake tokana na maelekezo ya aliyemshuhudia waliichora, walimtafuta na walimkamata?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kimsingi wengi wao hawana utu kutokana na kua na uwezo mdogo wa akili tena ukute na hofu ya Mungu hana ndo kabisa tunapata kilaza mwenye kibri kama Muna.
 
... eti aende kijijini mbali! Mbali ipi hiyo? Labda sio Tanzania. Unajua mabalozi wa nyumba 10 ni part of the security system ya nchi?
Wtu tumeenda visiwani huko na tumeishi vizuri tuu hata redio hazishiki, mimi naamini Tz kuna machimbo mengi ukifanikiwa kufika hawakupati ukituliza wenge.
 
Huyu mwamba alifia angani alivyoruka mkuu according to FBI.
Ok; the point is matokeo ya uhalifu ni mawili ama udakwe au ujiue/uuliwe. Ni wachache mno wanakwepa hayo mawili na Kato kwa vigezo vyovyote vile hana huo uwezo wa kuvikwepa.
 
Ok; the point is matokeo ya uhalifu ni mawili ama udakwe au ujiue/uuliwe. Ni wachache mno wanakwepa hayo mawili na Kato kwa vigezo vyovyote vile hana huo uwezo wa kuvikwepa.
Angefanikiwa kuvuka border chance ya kumkamata ingekua ndogo kama ni muhuni kweli.
 
Polisi hawana hiyo mitambo.

Ila Wana access ya kuomba taarifa za watu kwenye mitandao ya simu
 
Mission accomplished, kumkamata Kato hakurudisha Muna back to life
Natamani marehemu Afande Muna angewaza hili kabla ya kumfanyia ubabe Rasta Mayele.
Muuwaji kakamatwa aliyekufa hatorudi duniani, kabla hujapigana au hujampiga mtu fikiria mara mbili. Usiache cheo au dhamana ya kazi yako vikupe kiburi na kumdharau mtu.
Anaweza kukuuwa ukakosa matamu ya dunia, ukawaacha familia yako wakiteseka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…