2013 kwetu tulipata kibarua wa shamba, yule bwana kumbe huko kwao aliua jamaa mwenzie wakiwa kibanda umiza huko Tabora,
Yule bwana alikua mtiifu wa kazi za shamba na kuchunga mifugo yetu,
Alikaa pale kijijini had 2016 akaoa na kuanzisha familia yake, 2019 kuna jamaa mnunua mazao kumbe ni wa huko kijijini kwao na anamfahamu, alivyofika kumuona alihamaki, kakuta mwenzake ana mke na mtoto na nyumba yake, kiufupi ana maisha yake,
Yule jamaa ndo akatusimulia pale home, nakumbuka mzee akamuambia yule mgeni asiseme kwa watu, huwezi amini baada ya muda ndugu wa yule kibarua walikuja kule kijijini, navyoongea maisha yake yako pale kijijini ana fuga ng'ombe na mbuzi, kurudi kwao hataki tena, ila ndugu zake ndo wanamtembelea.