Kukamatwa kwa kiwanda bubu cha mafuta ya mawese mkoani Pwani, nawapongeza Zitto na Bashe kwa hatua walizochukua

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Jana iliibuka story mitandaoni ya Jeshi la Polisi kumkamata Mtanzania Halali akikamua Mafuta bila kuwa na "usajili" yaani vibali, Mafuta ya mawese. Kama kawaida Jeshi letu (ambalo kwa mujibu wa Waziri wake, wengi wao ni failures) hawakumuumiza kichwa Wala kutumia busara, wakaitisha Press na kumsulubu mwekezaji mzawa aliyekua anatafuta ada za watoto wake kwa njia Halali.

Mungu akitaka kukupa kitu sometimes anakupitisha Kwenye majaribio magumu sana, Police bila kujua kuwa kwa kuitisha Press walikua wanamsaidia kumpiga chura Teke. Leo ndugu Zitto alipost Twitter akimuonba Waziri wa Kilimo Husein Bashe kumsaidia mwekezaji mzawa huyu kujua hatua stahiki za kuboresha kazi yake na hatimae Bashe ameripoti kuwa ameshachukua hatua.

Jambo hili linastahili pongezi sana maana ni Watanzania wengi sana wanaumizwa na Hawa Watawala wadogo wanaojiita miungu Watu wakiongozwa na Jeshi la Polisi, Watendaji, na maafisa wengine wa SERIKALI.

---

Ujumbe wa Zitto Kabwe

Wananchi wanatafuta njia zao za kujipatia kipato. Bwana Halifa Issa anapaswa kusaidiwa kuonyeshwa njia za vibali na sio kukamatwa. Waziri wa Kilimo ndugu @HusseinBashe na Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Masauni kemeeni mambo haya. Huyu anafanya value addition. Support him

Majibu ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Nashukuru kwa Taarifa hii nimewasiliana na Mh DC wa kibaha nimemuomba amtafute huyu mwananchi na kumsaidia kupitia SIDO na wizara ya kilimo tuna promote “Value addition” through backyard processing hana tofauti na wale wa alizeti wanaouza Barabarani ni Jukumu letu kuwasaidia

CHANZO CHA SAKATA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limefanya msako mkali na kufanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Halifa Issa (42) mkazi wa Kongowe Wilayani Kibaha kwa kosa la kumiliki na kuendesha kiwanda bubu cha kuchakata mafuta ya mawese bila ya kuwa na kibali kinyume na sheria.
20220119_051646.jpg
20220119_051644.jpg
20220119_051641.jpg

Capture 1.PNG

Capture 2.PNG
 
Hivi viwanda viwe vingi tu, tena viindolewe Kodi zoote, VAT inatosha sana kwa serikali Kwa sekta kama hizi,

Ubunifu hapa, ni kulazimisha kiwanda kiajiri rasmi at least 2people (NSSF plus NHIF) included kwenye malipo Yao na mshahara uwe atleasrt official kima cha Chini cha serikali,

Wakikizi vigezo wasamehewe Kodi zoote za uendeshaji, ibaki VAT kwa whole saler wa product.

Ukifanya hivi utashanga kuna viwanda visivopungua 1M ambavyo vinasajiliwa officially,

Then utaongeza ajira, viwandani, mashambani, na utapunguza bei ya bidhaa Kwa mlaji WA mwisho maana viwanda vitakuwa vingi then vitashindani on price and quality na kumnufaisha mkulima.
 
Hamna kitu hapo ni usanii tu, tunaitaji sera bora na rafiki kwa watu kama hawa ni kweli wapo wengi sana, lakini kama mwekezaji mkubwa tu anakwamishwa na mifumo yetu ya kishamba huyo mdogo ataweza.
 
Kumiliki kiwanda bila ya kibali/leseni ni kosa kisheria. Lakini pia kuzalisha bidhaa kiwandani na kuuza pasipo kukagaguliwa na TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY nayo ni kosa kisheria na bidhaa hizo zaweza kuwa ni hatari kwa matumizi ya mwana wa Adamu.

Kwa mantiki hiyo huna sababu ya msingi ya kulilaumu jeshi la polisi. Kwani limetekeleza wajib wake. Bali kumpongeza mwana matukio Zitto na waziri wa kilimo ni jambo jema.

Ningekuona una maana endapo tu ungelisifu jeshi la polisi kwa kumwibua mhusika huo na akapata kusaidiwa na waziri wa kilimo.
 
Nazungumzia hili tukio, at least kumefanyika kitu otherwise mshkaji Mafuta yake yangeishia kwa wake wa Askari hao na yeye kupewa kesi mbaya
 
Hii tabia ya serikali na vyombo vya dola kuzuia, kudhibiti na kukamata wananchi wanaofanya ubunifu kwa kuongeza thamani au kutengeneza bidhaa inatakiwa ibadilishwe kwa kuwa na mtazamo chanya.
Uzuiaji, udhibiti na ukamataji huu ni uendelezaji wa fikra za kimasikini na rushwa.
Ili taifa liendelee hii tabia lazima ikome.
Pongezi kwa Waheshimiwa Waziri na Zito.
 
Kumiliki kiwanda bila ya kibali/leseni ni kosa kisheria. Lakini pia kuzalisha bidhaa kiwandani na kuuza pasipo kukagaguliwa na TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY nayo ni kosa kisheria na bidhaa hizo zaweza kuwa ni hatari kwa matumizi ya mwana wa Adamu.

Kwa mantiki hiyo huna sababu ya msingi ya kulilaumu jeshi la polisi. Kwani limetekeleza wajib wake. Bali kumpongeza mwana matukio Zitto na waziri wa kilimo ni jambo jema.

Ningekuona una maana endapo tu ungelisifu jeshi la polisi kwa kumwibua mhusika huo na akapata kusaidiwa na waziri wa kilimo.
Hapa tujiulize aina ya uhalifu wanaorusiwa kufanya na pia weledi wao katika kufanikisha majukumu ya ukamataji. Je wanao weledi na ruhusa ya kukagua viwanda? Je Polisi wanaruhusiwa kufanya ukaguzi viwandani? Wanao weledi wa kufahamu yapasayo kufanywa wakati wa ukaguzi?
 
Kufuata taratibu na sheria ndio msingi wa afya na usalama wa mlaji

Huyu mtanzania aliyeweza hadi kuwa na kiwanda bila kufuata utaratibu alikua na nia gani? ! Je ni kweli hajui kwamba ni makosa? Ubora wa bidhaa anayozalisha kibiashara ukoje?

Kusema kwamba police wamemuonea sio sawa, binafsi nawapongeza kwa kufanya kazi yao.

Kuendelea kushabikia uvunjifu wa sheria ati sababu alichofanya mtu kina manufaa tutakuja shangaa tunalishwa sumu na kuja kufa au kupata maradhi
 
Asante sana
 
Yote
Kumiliki kiwanda bila ya kibali/leseni ni kosa kisheria. Lakini pia kuzalisha bidhaa kiwandani na kuuza pasipo kukagaguliwa na TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY nayo ni kosa kisheria na bidhaa hizo zaweza kuwa ni hatari kwa matumizi ya mwana wa Adamu.

Kwa mantiki hiyo huna sababu ya msingi ya kulilaumu jeshi la polisi. Kwani limetekeleza wajib wake. Bali kumpongeza mwana matukio Zitto na waziri wa kilimo ni jambo jema.

Ningekuona una maana endapo tu ungelisifu jeshi la polisi kwa kumwibua mhusika huo na akapata kusaidiwa na waziri wa kilimo.
Yote uliyoyaandika ninakubaliana nawe isipokua aya ya kulisifu jeshi la polisi,tabia hii sijui itaisha lini hapa nchini why police wakimbilie press kabla ya kufanya uchunguzi kwanza na kujidhihirisha kwanza kosa lililofanyika na kumpeleka mahakamani kwanza?elewa alikua suspect!sio haki kwa polisi to parade someone bila y ushahidi wa kutosha.
 
Kufuata taratibu na sheria ndio msingi wa afya na usalama wa mlaji

Huyu mtanzania aliyeweza hadi kuwa na kiwanda bila kufuata utaratibu alikua na nia gani? ! Je ni kweli hajui kwamba ni makosa? Ubora wa bidhaa anayozalisha kibiashara ukoje?

Kusema kwamba police wamemuonea sio sawa, binafsi nawapongeza kwa kufanya kazi yao.

Kuendelea kushabikia uvunjifu wa sheria ati sababu alichofanya mtu kina manufaa tutakuja shangaa tunalishwa sumu na kuja kufa au kupata maradhi
Katika majukumu ingalikuwa vema polisi wakawashirikisha wenye mamlaka na weledi wa kukagua ubora wa chakula na kudhibiti uzalishaji wa bidhaa. Kwa kuwa wao hawakutaka kushirikisha hizo mamlaka husika ndipo linapokuja suala la NIA na DHAMIRA ya Polisi katika huo UKAMATAJI haukuwa sahihi na umejaa MASHAKA. Je wanao WELEDI? Je ni MCHONGO?
 
Hivi viwanda viwe vingi tu, tena viindolewe Kodi zoote, VAT inatosha sana kwa serikali Kwa sekta kama hizi,

Ubunifu hapa, ni kulazimisha kiwanda kiajiri rasmi at least 2people (NSSF plus NHIF) included kwenye malipo Yao na mshahara uwe atleasrt official kima cha Chini cha serikali,

Wakikizi vigezo wasamehewe Kodi zoote za uendeshaji, ibaki VAT kwa whole saler wa product.

Ukifanya hivi utashanga kuna viwanda visivopungua 1M ambavyo vinasajiliwa officially,

Then utaongeza ajira, viwandani, mashambani, na utapunguza bei ya bidhaa Kwa mlaji WA mwisho maana viwanda vitakuwa vingi then vitashindani on price and quality na kumnufaisha mkulima.
Wazo zuri mkuu
 
Back
Top Bottom