Sprouts pre School
Member
- Jul 15, 2026
- 64
- 187
Umoja wa wanataaluma chuo kikuu cha Dodoma (UDOMASA) umetoa taarifa ya kukamatwa kwa mwanataaluma mwenzao kwasababu ya tuhuma za kuhamasisha maandamano tarehe 7/7/2026.
Taarifa kutoka UDOMASA zinasema kuwa tarehe 3 Julai, 2026, Bw. Melkisedeki Kitunzi Kaijage alipokea wito kupitia mkuu wake wa idara akitakiwa kuripoti katika Kituo cha Polisi cha UDOM na tarehe 8 Julai, 2026 alitekeleza wito huo. mhadhiri huyo aliripoti kituoni hapo akiambatana na viongozi wawili wa UDOMASA na mwanasheria wake.
Jioni ya tarehe 8 Julai, Bw. Kaijage alipelekwa ofisi ya RCO kwa ajili ya kutoa maelezo. Ni wakati huo, ndipo viongozi na mwanasheria walipobaini kuwa mhadhiri huyo anatuhumiwa kuhamasisha maandamano ya tarehe 7 Julai, 2026.
UDOMASA inaripoti kuwa ingawa kosa hilo linalodaiwa lina dhamana, jaribio lao la kuomba dhamana lilikwama. Uongozi wa juu wa UDOMASA uliamua kuchukua hatua za kisheria kupitia njia ya mahakama.
Tarehe 12 Julai, 2026, walifungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma. Kesi hiyo ilisikilizwa jana, tarehe 17 Julai, 2026. Na baada ya kusikilizwa imeahirishwa na itasikilizwa tena Jumanne, tarehe 21 Julai, 2026 saatatu katika Mahakama Kuu Dodoma.
UDOMASA imelaani vikali kitendo cha kutomtendea haki muhadhiri huyo. Ikumbukwe pia Bw. Kaijage aliwahi kukamatwa baada ya maandamano ya tarehe 29 oct 2025 akituhumiwa kutumia darasa kushawishi wanafunzi kuandamana.
Pia ieleweke kuwa Kaijage anafundisha masomo ya siasa, na moja ya somo analofundisha ni PO 123 (Government and Politics in Tanzania) inayoongelea serikali na siasa za Tanzania baada ya uhuru hadi sasa. katika somo hili hana uwezo wa kukwepa kuongelea siasa za tanzania baada ya uhuru hadi sasa. kumuingilia katika ufundishaji wake kunaweza kuathiri elimu anayoitoa au akubali kuingia katika tuhuma hizo mara kwa mara.
Huko madarasani vyuoni huwa kuna maafisa vipenyo waoga, wasiotaka ukweli usemwe.