makologoto
Member
- Sep 21, 2013
- 38
- 27
Mimi nchi yangu inanishangaza sana. Mara nyingi huwa inaingia gharama kununua mitambo ya kisasa tena kwa majigambo makubwa lakini mara nyingi huwa haitumiki. Majuzi tuliaminishwa kuwa serikali ilikuwa halali kutumia billioni 82 kukarabati ukumbi wa bunge la katiba, ikiwa ni pamoja na kufunga mitambo ya kisasa kabisa ya kielektroniki kwa ajili ya kupiga kura badala ya kunyosha mikono au kusema ndiyo na hapana. Lakini kwa masikitiko kabisa hakuna hata mjumbe mmoja amewakumbusha serikali na wajumbe kuwa mitambo ipo ya kupigia kura iliyokura hela za walipakodi waitumie. Sijui hiyo mitambo imewekwa kimapambo? Hivi kweli hicho kitufe cha kura si kinakuwa programmed tu ku register kura na akimaliza kinajizima kabisa kiasi kwamba mtu hawezi kupiga mara mbili. Labda mniambie hii kura ya siri inayopingwa na wengi wana ccm ni ya siri kielektroniki, karatasi au ikoje?