DASA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 1,031
- 302
- Thread starter
- #21
Kuna Watu wengi wana mushkila wa Qabz ya tumbo (Constipation) kwa kiswahili kukosa kufanya haja kubwa. Kuna sababu tofauti:
1- Kukosa kunywa maji
2- Kukosa kula kwa wakti
3- Kukosa kula vyakula vya maana
4- Kukosa kwenda chooni wakati unapojihisi unataka kwenda na kujizuia.
Na hii husababisha uvivu na viungo kuuma na pia kujiona saa zote unataka kulala.
VIPI KUJITIBU BILA YA KUTUMIA HALULI
1- Kunywa maji gilasi 8 kwa siku
2- Kula kwa wakti wake.
3- Kula vyakula vya maana sio unaokotea tu.
4- Uwende chooni wakati unapojihisi unataka kwenda na usijizuie.
5- Kunywa maji baina ya kila tonge 2 au 3.
6- Kunywa mafuta ya Halzet (Olive Oil) au kutia kwenye chakula kama salad kila siku inasaidia kulainisha tumbo.
7- Kunywa maji kama gilasi 3 au 4 kisha ukawa unakwenda ukirudi kwa muda wa robo saa au dakika 20.
8- Kuchukua chupa ya Tanuf (litre 1 na nusu) na kutia chumvi kidogo kisha ukaichanganya sawa sawa halafu ukainywa yote kwa pamoja na hii mtu akifanya mwezi mara moja kwani kama haluli.
9-Kila Asubuhi na usiku - gilasi ya maji ya moto moto utachanganya na kijiko kikubwa cha asali na utakunywa.
10-Haba Sawda utasaga na uchanganye na asali na uwe unakula kijiko asubuhi kijiko usiku kila siku.
11- Fruits - Papai , Embe, Machungwa na kama unaweza ule maganda meupe.
12- Kwa watoto wadogo - juice ya chungwa - sukari na maji - asali na maji moto moto.
Fuata ushauri wangu Kisha unipe Feedback
Nitajitahidi mjomba!! Lakini mmh! zingne hapo mbona ngumu, watu wanazifanya kweli!! glass nane kwa siku..... etc, kwa muda gani.