SI KWELI Kukata kiuno ni hatari, huweza kusababisha ukapata ganzi mara kwa mara

SI KWELI Kukata kiuno ni hatari, huweza kusababisha ukapata ganzi mara kwa mara

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Salaam ndugu zangu,

Nimekutana na video fupi ikieleza kwamba kukata mauno ni hatari, kunaweza kuwa kisababishi cha ganzi kwa mwilini.

Tazama Video hapa chini:


Je, kuna ukweli hapa?
---

1692795617526.png
 
Tunachokijua
Kukata kiuno ni kitendo cha binadamu kujongesha (kuzungusha) kiuno kwa mtindo tofauti tofauti. Binadamu huweza kukata kiuno kwa malengo tofauti tofauti ikiwamo kucheza muziki au kufanya mapenzi. Kukata kiuno huweza huweza kufanya na mwanaume au mwanamke.

Kumekuwapo na hoja katika mitandao ya kijamii kuwa kitendo cha kukata kiuno ni hatari kwa sababu kinaweza kupelekea mishipa iliyo katika uti wa mgongo kugandamizwa na hivyo kupelekea kutokea ganzi.

Upi ukweli wa Jambo hili?
JamiiForums imefanya mawasiliano na Dkt. William Mgisha ambaye ni Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) ambaye amekanusha hoja hiyo na kutoa ufafanuzi wake wa kataalamu kama ifuatavyo:

Hakuna ukweli juu ya hilo lakini kuna madhara mengine yanayoweza kutokea kutokana na kucheza au kukata kiuno kwa miaka mingi, wahusika au mhusika anaweza kupata maumivu ya mgongo lakini sio ganzi.
Pamoja na hivyo, wanaopata Maumivu ya mgongo sio wengi, mfano kati ya professional dancer 10 anayeweza kupata changamoto hiyo ni mmoja.
Ganzi ya miguu inaweza kusababishwa na mabadiliko ya mgongo kutokana na umri au uchakavu wa pingili za uti wa mgongo.
Umri tunaozungumzia hapo ni kuanzia miaka 50+ japo wapo wenye umri wa miaka 40+ pia wanaopata changamoto kama hiyo.
Ushauri wa kitaalam kuhusu ganzi na maumivu ya mgongo, inashauriwa diet na ku-maintain uzito unaofaa, kwa kuwa vikienda tofauti vinaweza kuchangia maumivu ya mgongo na magoti.
Inashauri mtu mwenye miaka 50+ aende Hospitali angalau mara moja kwa mwaka kuangalia afya hata kama haumwi, itasaidia kutatua changamoto za magonjwa mbalimbali yaliyo hatua za awali.
Hivyo, kutokana na ufafanuzi huu wa kitaalamu JamiiForums inaona kuwa hoja ya kuwa kukata kiuno ni hatari na kunaweza kusababisha ganzi miguuni haina ukweli.
Back
Top Bottom