Kampuni ikiingia ICU kwa kushindwa kujiendesha tutalalamika?
Mkuu Icadon,
Ni vigumu sana kwa DAWASCO kuingia ICU kama itafanya biashara vizuri na wateja wakubwa kama taasisi ya jeshi.
Biashara yoyote kubwa, hata kama ya maji, inatakiwa iwe na utaratibu wa kukopesha wateja kwenye biashara hii inaitwa credit facilities. Ni vigumu kuwapata wateja wa fedha taslimu kila siku, otherwise kimizania taasisi za fedha kama benki zingeshindwa kufanya kazi, kwa kuwa wakopaji wasingekuwapo (tafadhali zingatia hapa). Kukopesha au kukopa si dhambi, bali ni utaratibu wa kuhuisha biashara.
Hata makampuni makubwa kama ya magari, ndege nk nayo huwa yanawakopesha wateja bidhaa zao na suala la ICU huwa halipo. Scania Tanzania, kwa mfano, wanawakopesha wateja wao magari hapa kwa kuwa wanatambua hilo. Biashara bila mikopo haiwezekani, labda iwe ya bidhaa ndogo ndogo sana.
Kwa kesi ya Dawasco na Jeshi, mteja alikuwa ameshalipa sh milioni 690, kati ya bilioni 1.2 ambazo zilitolewa kwenye bajeti ya maji na serikali. Zilizobaki zikalipwa kwenye taasisi za maji mikoani, kwa mujibu wa taarifa ya jeshi. Kwa hali hii, ni wazi kuwa jeshi lime exhaust fedha yote.
Hata kama suppliers wangetaka kukata maji, wangeheshimu unyeti wa taasisi yenyewe, ukizingatia kuwa ndiyo yenye dhamana ya kulinda mipaka ya nchi masaa 24 kwa kutumia rasilmali zetu zilizopo, maji yakiwemo. Wangefanya mawasiliano kuhakikisha kuwa deni linalipwa, na maji hayakatwi. Naamini hili lingewezekana, maana limewezekana pia hata sasa baada ya maji kukatwa.
Kwa kazijamii, jeshi pia linasaidia katika huduma za afya na elimu (naona wengi wetu hili hatulithamini, tunafika mahali tunakejeli kwani jeshi lina kazi gani!)Jeshi ilibaki kidogo sana liifunge hospitali ya Lugalo kwa kukosa maji wakati wa mzozo huu.
Najua wengi hatuna picha ya nchi ikiwa vitani inakuwaje. Ni vigumu kuona umuhimu wa ulinzi hadi nchi inapokuwa imevamiwa, na jeshi linakwenda vitani. Lakini pia haliwezi kuonekana liko kazini (vitani) wakati wa amani. Umuhimu wa kuwa na silaha, angalau mkuki au panga chumbani kwako utauona pale tu wanapokuvamia vibaka na mapanga, unapotumia zana hizo kujiokoa.
DAWASCO wanaweza kuingia ICU wakiwakatia maji wateja wakubwa kumi tu kama jeshi, ambapo nao wataamua kuchimba visima vyao au kuweka mitambo yao mtoni kuvuta maji.
Wanajeshi walipowapiga raia ni kitendo cha kinyama pia, hakistahili kupongezwa.
Jeshi ni la wananchi na linalelewa na serikali, na halifanyi biashara ya kuweza kujiendesha lenyewe. DAWSACO ni taasisi ya umma huo huo wa waTanzania, na ni ya kibiashara. Si kweli kwamba wamefikia mahali pa kilikatia jeshi maji kwa kuwa ni wadaiwa. Kuna sababu zaidi ya hizo, na nadhani tutazijua hivi karibuni.