Kukatisha matangazo Mubashara ITV dhidi ya mkutano wa ACT Zakhiem

Kukatisha matangazo Mubashara ITV dhidi ya mkutano wa ACT Zakhiem

Tarehe 19 Februari 2023 chama cha ACT Wazalendo walifanya mkutano wao wa Kwanza ambapo viongozi wake wa kitaifa walishiriki na kuongea na wananchi...
Pia ukumbuke kila chombo kina wasimamizi ambao,huweza kuwajibishwa pale ambapo wataruhusu maudhui "content" ambazo ni za kipotoshaji kurushwa hadharani.

Ndege za ATCL zinapitia hujuma kubwa toka kwa kundi la walamba asali.

Kwa kusudio la kuvuruga legacy ya Magufuli.
Chombo makini kama ITV hakiwezi kuuacha ujinga huo uendelee kupitia kituo chao.
 
Hakuna aliyekatiwa matangazo acheni kulalamikia mambo ambayo hayapo , Ni Zitto mwenyewe ameshindwa kupangilia hoja zake kwa kuzingatia muda, badala ya kushusha nondo mapema yeye kasubiria dakika za lala salama huku akijua kabisa muda waliolipia kurushwa Live utakuwa umekwisha na yeye atakuwa hajamaliza mazungumzo yake
 
Hivi hujui sheria za mikusanyiko mwisho ni sasa 12 jioni next time uwaeleze wasanii wa siasa waweke mambo ya msingi mapema sio kama ibada za kilokole.

USSR
Msanii wa kwanza ni Lema, mmekata moto mmerudi ubelgiji, no content.
 
Hizo ndege mnazolalamikia ndo mnazoongoza kuzipanda aiseee Zitto aje aongelee zile mil 15 za yanga je ni za mfukoni kwa Mama au za umma?
Anaweza kutoa mfuko wake wa kushoto akajirejeshea kwa mfuko wa kulia
 
Tarehe 19 Februari 2023 chama cha ACT Wazalendo walifanya mkutano wao wa Kwanza ambapo viongozi wake wa kitaifa walishiriki na kuongea na wananchi...
Kwani kulikuwa na ITV peke yake? Mabeberu je, CNN na BBC ni marafiki wa Zitto?
 
Hii ndio JF,Mwisho tunamaliza na habari za simba na yanga.
 
Tarehe 19 Februari 2023 chama cha ACT Wazalendo walifanya mkutano wao wa Kwanza ambapo viongozi wake wa kitaifa walishiriki na kuongea na wananchi.

Cheche zilianza kuonekana pale aliposimama Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar ambape pia ni makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar alipoelezea umma kuhusu ACT kuanzisha mchakato wa maridhiano ambao ulikuja baadaye kuwashirikisha CHADEMA lakini hilo halijawahi kusemwa popote.

Alisimama Mwenyekiti wa Taifa wa ACT ambaye naye alielezea miaka 7 ya giza ambapo vyama vilisitishwa kufanya shughuli zake za kisiasa, vyombo vya habari kutishiwa na kushughulikiwa endapo vitatoa habari zinazoikosoa serikali. Lakini hata waandishi na wanachi walioonesha mwelekeo huo walishughulikiwa kikatili na serikali.

Hatimaye alisimama mzee wa Terrible Teens yaani Kiongozi mmkuu wa Chama bwana Zitto ambaye bila hiyana alipita mulemule kuuelezea umma maswahibu ya wananchi kutokujua matumizi na udhibiti wa kodi zao hadi kununua madege ambayo mengine yapo grounded kwa sababu ya kutu.

Alipoanza kuelezea details za namna fedha za ndege zilivyotengwa na kununuliwa ndipo ghafla ITV walikata matangazo yao ambayo hapo awali tuliambiwa yatakuwa live hadi mkutano utakapoisha.

Hii ina maana kubwa sana. Inamaanisha kuwa pamoja na juhudi za Mama Samia kutuelezea namna anavyouthamini uhuru wa vyombo vya habari na vyama vya siasa kufanya shughuli zao, lakini kiuhalisia kazi bado sana na uhuru huo unaotolewa una mipaka yenye miba mikali.

Kinachofuatia ni ITV kuanza kumulikwa vikali na taasisi ya vipenyo na huko mbeleni msishangae wakapigwa dafrao kali huku mkishindwa kuunganisha nukta za tukio la jana.

Ninapinga vikali kitendo cha ITV kuamriwa kuuondoa matangazo ya live mkutano wa ACT Wazalendo pale Mbagala Zakhem siku ya tarehe 19 Februari 2023.

Huyo masoud Hana ya kuongea? Maridhiano walianzisha wait Kama akina Nani?. Kwa hivyo ACT ndio walianzisha maridhiano Kati ya CCM na CHADEMA. Waongi kweli
 
Sheria hiyo inatekelezwa kwa wapinzani pekee?

Mara ngapi hata hivi karibuni CCM wanapitisha mikutano yao hadi kuzidi muda wa saa 12 alasiri?

Majibu mepesi sana mnatoa
Ya ndani inaweza kwenda mpk usiku lkn ya hadhara mwisho saa 12. Labda uje na ushahidi wa mkutano wa hadhara wa ccm ulioenda mpk saa 2 usiku .
 
Ya ndani inaweza kwenda mpk usiku lkn ya hadhara mwisho saa 12. Labda uje na ushahidi wa mkutano wa hadhara wa ccm ulioenda mpk saa 2 usiku .
Labda uniambie nikupe ushahidi mkutano ulioisha ndani ya saa 12.

Na kama ACT walizidisha muda, tungesoma news polisi kusimamisha mkutano kwa kuvunja sheria ya muda wa mkutano.

Reasoning yetu ndani ya CCM haina tofauti na ya Thomaso mwanafunzi wa Yesu
 
Wacheni siasa za mipasho hizo.Hazina tija.Futa vyama vyote tutengeneze mfumo mwengine wa utawala si demokrasia na wala si ufalme.Kama tutashindwa kujiundia mfumo wetu basi afadhali tuchukue kidogo kutoka China.

Hapo kwanza uanze mchakato wa kuwa jimbo la china ili kupata ulinzi,kisha ndio tuanze kupambania huo mfumo mpya,vinginevyo kijani lazima watemeshwe bungo na mabeberu kitu ambacho wanaogopa sana.
 
Sheria hiyo inatekelezwa kwa wapinzani pekee?

Mara ngapi hata hivi karibuni CCM wanapitisha mikutano yao hadi kuzidi muda wa saa 12 alasiri?

Majibu mepesi sana mnatoa
Change asali mnazo lamba mfungue kituochenu cha tv.
 
Hapo kwanza uanze mchakato wa kuwa jimbo la china ili kupata ulinzi,kisha ndio tuanze kupambania huo mfumo mpya,vinginevyo kijani lazima watemeshwe bungo na mabeberu kitu ambacho wanaogopa sana.
Umeongea ukweli mchungu
 
Pia ukumbuke kila chombo kina wasimamizi ambao,huweza kuwajibishwa pale ambapo wataruhusu maudhui "content" ambazo ni za kipotoshaji kurushwa hadharani.

Ndege za ATCL zinapitia hujuma kubwa toka kwa kundi la walamba asali.

Kwa kusudio la kuvuruga legacy ya Magufuli.
Chombo makini kama ITV hakiwezi kuuacha ujinga huo uendelee kupitia kituo chao.
Well said mkuu,nandio kilicho fanyika.
 
Pia ukumbuke kila chombo kina wasimamizi ambao,huweza kuwajibishwa pale ambapo wataruhusu maudhui "content" ambazo ni za kipotoshaji kurushwa hadharani.

Ndege za ATCL zinapitia hujuma kubwa toka kwa kundi la walamba asali.

Kwa kusudio la kuvuruga legacy ya Magufuli.
Chombo makini kama ITV hakiwezi kuuacha ujinga huo uendelee kupitia kituo chao.
Serikali inayotuhumiwa na ikakaa kimya.maana yake ni kuwa tuhuma.hizo zina ukweli.

Kidhibiti ukosoaji ni.wazi anayekosolewa ndiye tatizo
 
Back
Top Bottom