The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 838
Ukraine imeonya kuwa kukatizwa kwa shehena za silaha za Marekani huenda kukachochea Urusi kuendeleza vita nchini humo, ambayo sasa ni mwaka wake wa nne.
Siku ya Jumanne Ikulu ya White House ilisema kuwa imekatiza baadhi ya silaha zinazopelekwa Ukraine.
Uamuzi huo ulichukuliwa "kuweka maslahi ya Marekani mbele" kufuatia uchunguzi wa Idara ya Ulinzi kuhusu "msaada wa kijeshi na usaidizi wa Marekani kwa nchi nyingine", msemaji wa Ikulu ya Marekani Anna Kelly alisema.
Wizara ya mambo ya nje ya Ukraine ilisema katika taarifa yake kwamba "kucheleweshwa au kuahirisha kuunga mkono uwezo wa ulinzi wa Ukraine kutahimiza tu Urusi kuendeleza vita na ugaidi, badala ya kutafuta amani."