WILLIAM MARCONI
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 2,108
- 878
Lowassa ameonewa kabisa,huyu bwana anafanya siasa za kimataifa kabisa kama marekani,tunaona wagombea wa urais marekani wanaanza harakati zao ndani ya chama muda mrefu sana na kujiandaa vyema...lakini kwa ccm siyo.yaani unamtaka yule ambaye atawafumbia macho....katika kundi hilo waote pale maamuzi yao yanatabirika....lowasa pekee ndiye alikuwa maamuzi magumu ambayo wakuu wa ccm hawapendi.....
Namshauri Lowassa.....nenda upinzani hasa Ukawa maana wana fremwork saffi.....ushinde urais...utapata kura za kumwaka ambazo watashindwa kuiba.
Wakati mwingine ni bora kukaa kimya..Lowassa alikuwa chaguo la wachumia tumbo, watumwa wa mali walopanda mbegu za magugu katika shamba la ngano na kuishi kwa matumaini - HOPE ya kwamba ONE day YES mbegu hizo zitaota baina yake na Ngano bila kugunduliwa. Wakasahau ya kwamba magugu kusubiriwa kwanza yakaota pamoja na ngano, kwa sababu huwezi ng'oa miche ya magugu pekee unaweza kung'oa hata miche ya ngano safi. Hivyo husubiria yakaota kisha kupaririwa na kuchomwa moto, watu wakavuna ngano safi na kuiweka Ghalani..
Katika mambo yote alowahi kufanya JK atakumbukwa zaidi kwa hili, na Heko CC ya CCM kwa kufanya maamuzi sahihi. Kusema kweli sitojali tena nani baina yao atakuwa rais wa JMT maadam sio Lowassa..
Nai akiingia ACT! Lowassa? huyu mwizi hawezi kujiunga ACT kwa sababu hana sifa za uongozi, pengine UKAWA maana ndio mtu pekee anayeweza kuwashinda CCM kwa sababu ya watumwa wengi wa akioli wapo huko. UKAWA wanachotaka ni kugawana kwa hiyo hii ime fit vizuri kwao. Lowassa alipendwa na UKAWA wote na muda wote dhidi ya JK..Vipi mkuu Akiingia ACT ya "kipenzi chako" Zitto utamsapport?
Nai akiingia ACT! Lowassa? huyu mwizi hawezi kujiunga ACT kwa sababu hana sifa za uongozi, pengine UKAWA maana ndio mtu pekee anayeweza kuwashinda CCM kwa sababu ya watumwa wengi wa akioli wapo huko. UKAWA wanachotaka ni kugawana kwa hiyo hii ime fit vizuri kwao. Lowassa alipendwa na UKAWA wote na muda wote dhidi ya JK..
Mkuu Lowassa toka mwaka 2005 alijulikana na kutishia kuhamia CDM huu ni muendelezo tu. Kwa nini UKAWA hawakutangaza mgombea wao hadi CCM watangaze kwanza walikuwa wanasubiri nini? Anyway Lowassa akikaribishwa ACT naachana na siasa za Bongo napaka kila kona..Kumbuka Zitto alisha mkaribisha, alisema Lowassa anakaribishwa iwapo akitangaza madeni na mali zake.
Wanabodi, CC ya CCM, imefanya kazi yake, imelikata jina la kipenzi cha wengi, Edward Ngoyai Lowassa!.
Jee kukatwa huku ndio mwisho wa ile safari ya matumaini, au ndio mwanzo wa safari ya kweli ya matumaini, kwa kipenzi cha watu, kuanza rasmi safari ya ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania, kwa kuipeleka rasmi CCM kaburini?
Kwa miaka 50 sasa, Watanzania tumelogwa na jinamizi la CCM kiasi cha kuamini mgombea wa CCM ndie automatically atakuwa rais wa Tanzania!. Wanaopiga kura sio CCM bali ni Watanzania!. Kama Lowassa ndie chaguo la watu, CCM wakaamua kumkata, jee sisi ambao ndio watu, tumchukue Lowassa, kupitia chama kingine chochote tumuingize ikulu?
Lowassa sema....
Sema usiogope sema!.
Linasubiriwa Neno tuu!.
Pasco!
Wanabodi,
Wapenzi, wafuasi, na mashabiki wa Lowassa, wanachosubiri sasa ni aseme neno moja tuu na roho zao zitapoa!, akiamua kukubali matokeo kuwa kukatwa kwake ndio mwisho wa safari, na akubali na aseme wazi, "Eloi Eloi, Yemekwisha!", na kama hajakubali, atamke wazi kuianza ile safari ya ukombozi wa pili wa Mtanzania, dhidi ya mkoloni mchwa CCM, aliyelitafuna taifa letu kwa miaka 50, na akitamka tuu!, "CCM Basi!", huo ndio utakuwa mwisho wa hili zimwi linaloitwa CCM!, CCM itakuwa ni bye bye jumla, kaburini forever!,
Lowassa sema....
Sema usiogope sema!.
Linasubiriwa Neno tuu!.
Pasco!
Mkuu Mp Kalix2, nayatafakari maneno haya kwa kina!.Kushiriki katika ukombozi kwa njia hiyo ni jambo ambalo anaweza kulifanya ili aweze kujitendea haki baada ya udhalilishaji mkubwa aliofanyiwa na wanamtandao na hasa Rafiki yake. "Hatuja kutana barabarani"
Hana cha kupoteza zaidi nikujijengea nafasi mpya mbele ya Safari kwani UKAWA watakuwa magogoni na kama ujuavyo Siasa ni Sanaa kwa hiyo kuwapo yeye kwenye vita ya Ukombozi lazima kuna zawadi /malipo anayostahili baada ya kazi kukamilika maana Majimbo kadhaa yaliyo ngome kuu za CCM watachukua yeye na Chama chake kipya.
huu ni muda kwa UKAWA kuwa na MOUDs na chama atakacho hamiana si kwa minajili ya kuungana bali kwa mikakati ya Ushindi dhidi ya goli la Mkono.
Mkuu , uliposema haya, ulimaanisha ni akikaribishwa ACT tuu au hata akikaribishwa UKAWA?!, ili tujiandae kusubiri hayo ..... yatakayopakwa kila kona?.Mkuu Lowassa toka mwaka 2005 alijulikana na kutishia kuhamia CDM huu ni muendelezo tu. Kwa nini UKAWA hawakutangaza mgombea wao hadi CCM watangaze kwanza walikuwa wanasubiri nini? Anyway Lowassa akikaribishwa ACT naachana na siasa za Bongo napaka kila kona..
Kifupi, Lowassa ni mtu mwenye KASHFA nzito nzito za uongozi ambazo anatakiwa kusimamishwa na hata kushtakiwa. Mbali na hilo ni mtu anayetaka uongozi by any means necessary! Kiongozi huchaguliwa na watu sio haki ya mtu. Hatakiwi mtu wa aina hii kupewa uongozi atakuwa na kisasi, ni wa kuogopwa kama Ukoma!..Mimi nilikuwa mwanachama wa CCM toka mwaka 1973, ni watu kama yeye waloniondoa imani na chama hicho...Mkuu , uliposema haya, ulimaanisha ni akikaribishwa ACT tuu au hata akikaribishwa UKAWA?!, ili tujiandae kusubiri hayo ..... yatakayopakwa kila kona?.
Pasco
Mkuu , uliposema haya, ulimaanisha ni akikaribishwa ACT tuu au hata akikaribishwa UKAWA?!, ili tujiandae kusubiri hayo ..... yatakayopakwa kila kona?.
Pasco