Kukira je kuna ukweli?

Long'ututi

Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
41
Reaction score
4
huwa nasikia eti mtu akijifungua kisha wazazi wa mtoto yeyote kati yao akiwa na uhusiano nje ya ndoa ili hali mtoto ananyonyeshwa humfanya mtoto alemae,awe kama ana mtindio wa ubongo na hatakua tena,kuna ukweli hapa au ni stori za mababu?
 
sijui,ngoja tuone wana jf wengine
 
huwa nasikia eti mtu akijifungua kisha wazazi wa mtoto yeyote kati yao akiwa na uhusiano nje ya ndoa ili hali mtoto ananyonyeshwa humfanya mtoto alemae,awe kama ana mtindio wa ubongo na hatakua tena,kuna ukweli hapa au ni stori za mababu?

ni stori tu mbona ata ww ungekuwa na mtindio
 
kwani nje ya ndoa mnatafutaga nini?
 
Hamna cha maana nje za ndoa,just napenda kufaham hiyo stori ni kwl au la!
 
Sio kweli bwana kama ni hivyo kungekuwa na walemavu na wenye mtindio wa ubongo wengi!!
 
huko ni kutishana tu! ili watu wajitambue na kuacha matendo maovu!
 
So kumbe ni stori tu..Ila watu wa lugha husema kila msamiati huundwa kutokana na ukwl uliopo kwenye jamii sasa kwanini maneno kubemendwa au kukirwa yapo katika jamii?
 
Kisayansi si kweli. Lengo ni kujenga maadili mazuri.
 
Hii ilitumiwa na wabibi ili watu wasitoke nje ya ndoa na watumia muda kutunza watoto. Watoto kuanzia miezi sita mahitaji yao ya virutubish huongezeka na asipopata proper feeding(quality, quantinty,feeding frequency,) na huduma bora za afya inapelekea kupata utapiamlo. Marasmus (unyafuzi) ukosefu/upungufu wa nishati mwilini na husababisha metabolic activities kuwa slow. KWASHIORKOR ni ukosefu/upungufu wa protein mwilini. Pia hivi huambatana na micronutrient deficiencies kama madini na vitamins. Kwa pamoja mtoto hukonda, nywele huwa za nyepesi za gold, kitumbo cha chinichini, ****** hutepeta na kuning'inia, uso kama mbalamwezi, uzito mdogo kwa urefu wake,hana apetite ,kuvimba,kwa kwashiorkor, apetite kubwa kwa marasmus. Hii pia huathiri ukuaji na ufanyaji kazi wa ubongo. mtoto huwa mnyonge, anajitenga, hachezi, nk. Hapo ndio mama huambiwa kambemenda mtoto.
 


Wazee wa zamani walikuwa Philosophers kuliko kizazi cha sasa.
Kama kweli unampenda mwanao utapenda awe amekondeana, mnyonge, yuko hovyo hovyo. Kutokana na kutishwa kuwa ukitoka nje mtoto atakuwa hivyo mama atatulia nyumbania na mtoto, mtoto atapata matunzo bora na pia mama atajiepusha na magonjwa ya zinaa na mambo mengine!
 
kweli kabisa wazee wa zamani walikuwa wanafanya hivyo ili kulinda maadili ya jamii na watu watulie kulea watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…