Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari!
Twende kwenye hoja.
Mateja au kuongezeka kasi ya matumizi ya madawa ya kulevya serikali ndio chanzo kikuu.
Kwanini niseme serikali ndio chanzo kikuu cha tatizo hili?
Serikali ndio inayokusanya kodi, hizo kodi ndizo hutumika kuwalipa watumishi wa idara ya polisi, TISS, Uhamihaji, Tume ya kudhibiti madawa ya kulevya, PCCB, Mahakama n.k
Serikali imeshindwa kuviongoza vyombo hivi nilivyovitaja juu kukomesha uteja kwa vijana.
Ukifika asubuhi kesho Temeke Hospital utakutana na mateja mamia au maelfu wanapanga foleni kupokea Methodone (Dawa za kuondoka kiu ya uteja wa madawa ya kulevya).
Hivi serikali imeshindwa kudeal na mizizi ya tatizo kiasi hiki mpaka wanadeal na majani(mateja).
Hizi ni akili?
Serikali imeshindwa kuwakamata mateja angalau 5 waonyeshe mtu anayewauzia, kisha huyo mtu aminywe awapeleke kwa dealer mkuu wao?
Kisha dealer mkuu akipatikana na hatia afungwe maisha.
Tatizo hivyo vyombo juu havisimamiwi ipasavyo katika hili, badala yake wanawageuza ma pusher na mabosi wao kama kitega uchumi.