Kukithiri kwa mateja (Wala madawa ya kulevya) Serikali iwajibike maana ndio inayopelekea tatizo kuwa kubwa zaidi

Biashara ya dawa ni tofauti na biashara nyingine na ndio maana hata INCB kwenye vikao vyake kila mara wanajaribu kuboresha sera na mbinu za kukabiliana na athari za matumizi ya dawa (narcotics na pyschotropic substances) .
Kinachotokea ni “Matumizi mabaya” ya dawa husika maana miongoni mwa dawa zinazotumiwa vibaya zipo ambazo hata sasa hutumika kwenye tiba .
Ndio maana wazungu wanamsemo wao “Monkey on your back” yaani ukianza kutumia vibaya dawa hizi yaani si rahisi kuachana nazo kwa jitihada zako mwenyewe unahitaji msaada .
Tena kuna watu wengi wenye heshima kwenye jamii na wametumbukia kwenye hii kasumba ya uraibu na hawana msaada.
Ukiwa na ndugu au jamaa ambaye ni mraibu njia ya kumsaidia ni kumsimamia katika matibabu ya uraibu (methadone and behavior therapy) kisha akianza “get clean” mpatie shughuli na umsimamie mpaka hapo atakapo kaa sawa .
 
Mbona Makonda aliweza?

Acha kutetea ujinga

Makonda aliweza nini ? Anaingia kuwa mkuu wa mkoa kituo kimoja hapo dsm kilikuwa na wastani wa waraibu 200 na makadirio ilikuwa baada ya miaka mitano hiyo namba kupungua .
Unajua nini kilitokea ? Kituo kimoja kilikuwa na waraibu si chini ya 1000 mpaka sasa imelazimu kuongeza vituo zaidi ya vitatu dsm pekee scarcity ya wahudumu katika vituo hivi ndio changamoto kubwa .
Hakuna kitu makonda alifanya labda public stunt hajawahi kufika hata kwenye ground kuona ukubwa wa tatizo lenyewe !
 

binafsi makonda sikumpenda anapoongea,ilikuwa lazima atoe kauli zenye ukakasi,ila kwenye kazi sijawahi kutilia shaka.

mimi huwa nasema unafiki ni kansa inayotutafuna sana mpaka hatupigi hatua.
mtu anakemea madawa,ushoga,majukumu ya uzazi,anapigwa majungu mpaka wafadhiri wa ushoga wanamsakama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…