Kukokotoa faida na hasara kwenye biashara ya jumla na reja reja na namna nzuri ya kuuza

Kukokotoa faida na hasara kwenye biashara ya jumla na reja reja na namna nzuri ya kuuza

OgaBoy

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
1,531
Reaction score
2,140
Natambua mpaka mzigo uishe ndo tunaweza pata hesabu za faida na hasara vinginevyo itakuwa tuna assume tu. Ila kama inawezekana unaweza nipatia formula ili nione inavyokuwa.

Kuna hizi bidhaa hapa

Bidhaa zinazokuwa kwenye package moja ila zinauzwa moja moja labda ndani ya package ziko mia na zilinunuliwa kwa 2000 na kila kimoja kinauzwa kwa shilingi 50 ambapo vikiisha faida inakuwa 3000.

Je kama nimeuza 10 kwa siku na vikabaki 80 naweza kokotoa faida au nivumilie mpaka viishe

Si mtaalamu kwenye kuuza au biashara pia nisaidie kuhusu kuuza kiisahihi
 
Mbona nyepesi hio mkuu....

Jumla ya faida ni 3000 ukiuza zote 100.
Kwahio kwa kila piece ni 30 kwa kila piece.
Kama umeuza piece 40; 40×30=1200 ambayo ni faida ya pieces 40.

Kula tu faida, usije nyemelea mtaji
 
Bado hujajibu hoja ya muuliz swali
 
Yaah, kalukulate mkuu

Mfano package yenye vitu 10
Vitu 10 faida ni 3000
Ko unachukua 10x3000 unazidisha na faida 10
Ko hapo ukiongeza na kodi unapata hela nzuri tu😇
 
Vumilia mpk uone ulivyouza vimerudisha hela uliyonunulia baada ya hapo vitavyobaki ni faida. So utaamua utumie mwenyewe au uuze
 
Natamani kujua haya maduka makubwa bidhaa zimejaa na wana wafanyakazi, wanakokotoa vipi hesabu bila kupigwa
 
Jumla pekee ambayo Haina rejareja unaweza kujua faida,maduka ya rejereja ni vigumu mno kucalculate faida,Kwa duka la jumla unaweza ukajua faida kwa kuhesabu bidhaa ulizokuwa nazo pindi unafungua na bidhaa zilizobaki pindi unafungua.
 
Nina duka la nguo utaratibu wangu ni huu:

Huwa narekosi kwenye daftari mauzo ya kila bidhaa na jioni kuhamishishia kwenye software (excel)

Kila nguo najua nimeinunua sh ngapi, hivyo kila nguo lazima nitoe sh 2000 ya uendeshaji wa ofisi. Kila mwezi nafunga hesabu na kuanza mwezi mwingine. Mwisho wa mwezi nakua najua mambo haya kupitia hio excel:

1. Nimeuza pc ngap
2. Jumla ya mauzo ni sh. gani
3. Matumizi ya ofisi (kununua mzigo) ni sh. gap

4. Matumizi ya ofisi yasiyo ya kununua mzigo (mf. taka, tra, nk) ni sh ngap

5. Tofauti ya mauzo na manunuzi ni sh ngap

6. Matumizi binafsi ni sh ngap
Nk

Salio linalobaki bank nahama nalo mwezi unaofuata.

Yote hayo huchakatwa automatic na excel

Budhaa za package kama boxer na vest huwa sizipigii hesabu za faida. Huwa naziingiza kwenye mauzo bila kuchakata faida yake maana zenyewe huwa nazichulia kama nyongeza kwa wateja. Mfano mteja kanunua nguo za laki zinazokupq faida ya 20k. Akachukua na vest moja au boxer moja yenye faida ya 1k. Hii boxer huwa sihesabu kuwa ni bidhaa ya kunipa faida ila itaingia kwenye mauzo.

Bidhaa hizi kama boxer na vest na mikanda na sock na kofia, kama mteja kanunua mzingo mkubwa wa kunipa faida huwa namuuzia hata kwa bei niyonunulia. Lengo ni kulinda mtaji na wateja wasikose bidhaa.

Nawasilisha
 
Nikuambieni kitu kimoja siri ya kufanikiwa kwenye biashara ni ubahili tu achana na hizo blablah mara ohh narekodi kila pc mara mwingine nahesabu idadi
 
Nina duka la nguo utaratibu wangu ni huu:

Huwa narekosi kwenye daftari mauzo ya kila bidhaa na jioni kuhamishishia kwenye software (excel)

Kila nguo najua nimeinunua sh ngapi, hivyo kila nguo lazima nitoe sh 2000 ya uendeshaji wa ofisi. Kila mwezi nafunga hesabu na kuanza mwezi mwingine. Mwisho wa mwezi nakua najua mambo haya kupitia hio excel:

1. Nimeuza pc ngap
2. Jumla ya mauzo ni sh. gani
3. Matumizi ya ofisi (kununua mzigo) ni sh. gap

4. Matumizi ya ofisi yasiyo ya kununua mzigo (mf. taka, tra, nk) ni sh ngap

5. Tofauti ya mauzo na manunuzi ni sh ngap

6. Matumizi binafsi ni sh ngap
Nk

Salio linalobaki bank nahama nalo mwezi unaofuata.

Yote hayo huchakatwa automatic na excel

Budhaa za package kama boxer na vest huwa sizipigii hesabu za faida. Huwa naziingiza kwenye mauzo bila kuchakata faida yake maana zenyewe huwa nazichulia kama nyongeza kwa wateja. Mfano mteja kanunua nguo za laki zinazokupq faida ya 20k. Akachukua na vest moja au boxer moja yenye faida ya 1k. Hii boxer huwa sihesabu kuwa ni bidhaa ya kunipa faida ila itaingia kwenye mauzo.

Bidhaa hizi kama boxer na vest na mikanda na sock na kofia, kama mteja kanunua mzingo mkubwa wa kunipa faida huwa namuuzia hata kwa bei niyonunulia. Lengo ni kulinda mtaji na wateja wasikose bidhaa.

Nawasilisha
na uhitaji wa kujua namna ya kuingiza DATA kwenye Excell mkuu,naomba msaada wa hata mFano wa namna unafanya wewe.
 
Back
Top Bottom