Nina duka la nguo utaratibu wangu ni huu:
Huwa narekosi kwenye daftari mauzo ya kila bidhaa na jioni kuhamishishia kwenye software (excel)
Kila nguo najua nimeinunua sh ngapi, hivyo kila nguo lazima nitoe sh 2000 ya uendeshaji wa ofisi. Kila mwezi nafunga hesabu na kuanza mwezi mwingine. Mwisho wa mwezi nakua najua mambo haya kupitia hio excel:
1. Nimeuza pc ngap
2. Jumla ya mauzo ni sh. gani
3. Matumizi ya ofisi (kununua mzigo) ni sh. gap
4. Matumizi ya ofisi yasiyo ya kununua mzigo (mf. taka, tra, nk) ni sh ngap
5. Tofauti ya mauzo na manunuzi ni sh ngap
6. Matumizi binafsi ni sh ngap
Nk
Salio linalobaki bank nahama nalo mwezi unaofuata.
Yote hayo huchakatwa automatic na excel
Budhaa za package kama boxer na vest huwa sizipigii hesabu za faida. Huwa naziingiza kwenye mauzo bila kuchakata faida yake maana zenyewe huwa nazichulia kama nyongeza kwa wateja. Mfano mteja kanunua nguo za laki zinazokupq faida ya 20k. Akachukua na vest moja au boxer moja yenye faida ya 1k. Hii boxer huwa sihesabu kuwa ni bidhaa ya kunipa faida ila itaingia kwenye mauzo.
Bidhaa hizi kama boxer na vest na mikanda na sock na kofia, kama mteja kanunua mzingo mkubwa wa kunipa faida huwa namuuzia hata kwa bei niyonunulia. Lengo ni kulinda mtaji na wateja wasikose bidhaa.
Nawasilisha