Kukokotoa punguzo la bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwa mwezi wa sita 2022 baada ya kuongezewa ruzuku ya billioni 100 (100B)

Hivi data za TRA unazipataje mkuu. Mimi hizi data nazitafuta sana.
Zinafichwa kwa sababu wanazozijua wao ili tuendelee kupigika. TRA ndiyo wanakusanya kodi za mafuta yanayoingia nchini bandarini kwa matumizi yetu na yale ya transit kila siku. Hawataki kuweka takwimu hizi public.

Na tutaendelea kutumia price peak ya March 2022 ya USD 139 per barrel of crude oil ambayo ilidumu kwa siku chache tu. Kuanzia April 2022 bei haijazidi USD 107 kwa pipa.

Haya bei mpya EWURA wameshatoa. Punguzo ni Sh 107 tu wakidai mafuta yanayokuja na yatakayokuja mwezi wa July yalinunuliwa mwezi March 2022. Ni bongoland.
 
Mbona kama punguzo ni 306 Tsh mkuu.
 
Nanukuu maelezo ya waziri wa nishati Mh. January Makamba ili hesabu zangu ziende vizuri.

"Waziri Makamba aliongeza kuwa hadi kufikia Aprili 1, 2022 petroli iliyokuwa kwenye maghala ni jumla ya lita 118,594,024 yanayotosheleza siku 27, dizeli lita 116,486,705 yanatosheleza siku 19, Mafuta ya taa lita 6,823,710 yanatosheleza siku 108 na Mafuta ya ndege lita 12,841,822 yanatosheleza siku 35.

Hivyo matumizi ya petroli kwa siku 30
= (lita 118,594,024 Γ— 30) Γ· 27
= lita 131,771,137.778 za mafuta ya petroli kwa siku 30

Hivyo matumizi ya dizeli kwa siku 30
= (lita 116,486,705 Γ— 30) Γ· 19
= lita 183,926,376.316 za mafuta ya dizeli kwa siku 30

Hivyo matumizi ya mafuta ya taa kwa siku 30
= (lita 6,823,710 Γ— 30) Γ· 108
= lita 1,895,475 za mafuta ya taa kwa siku 30

Hivyo matumizi ya mafuta ya ndege kwa siku 30
= (lita 12,841,822 Γ— 30) Γ· 35
= lita 11,007,276 za mafuta ya ndege kwa siku 30

Tuhakikishe kama kweli hesabu zetu kama zimekwenda sawa kupitia maelezo ya Mh January Makamba. Nanukuu

"Vilevile kuna meli ambazo zimewasili nchini na zinaendelea kushusha mafuta zikiwa na lita 86,256,000 za dizeli. Hivyo kwa kuzingatia mafuta yaliyokuwepo tarehe 01 Aprili 2022 nchi itakuwa na jumla ya lita 202,742,705 za mafuta ya dizeli zitakazotosheleza matumizi ya nchi kwa siku 33."

Hivyo matumizi ya dizeli kwa siku 30
= (lita 202,742,705 Γ— 30) Γ· 33
= lita 184,311,550 za mafuta ya dizeli kwa siku 30

"hivyo nchi itakuwa na jumla ya lita 189,979,324 za mafuta ya petroli yakutosheleza siku 37".

Hivyo matumizi ya petroli kwa siku 30
= (lita 189,979,324 Γ— 30) Γ· 37
= lita 154,037,289.73 za mafuta ya petroli kwa siku 30


Hesabu za mafuta ya dizeli zimetofautiana kidogo hivyo inabidi tutafute wastani.

Wastani wa matumizi ya petroli kwa siku 30
= (lita 131,771,137.778+ lita 154,037,289.73)Γ·2
= lita 142,904,213.754 za mafuta ya petroli kwa siku 30

Wastani wa matumizi ya dizeli kwa siku 30
= (lita 183,926,376.316+184,311,550)Γ·2
= lita 184,118,963.158 za mafuta ya dizeli kwa siku 30

Kumbuka ruzuku ya billioni 100 (100B) iliyotolewa ni kwaajili ya mwezi mmoja tu (siku 30) na ni kwa mafuta ya petroli na dizeli tu.

Jumla ya matumizi ya petroli na dizeli kwa siku 30
= lita 142,904,213.754 za petroli + 184,118,963.158 za dizeli
Jumla = lita 327,023,176.912

Jumla ya Ruzuku iliyotolewa kwa mwezi (siku 30)
Tsh Billioni 100 = Tsh 100,000,000,000

Kumbuka bei ya mafuta haijabadilika katika soko la dunia mwezi wa sita.

Ruzuku kwa lita moja ya mafuta
Ruzuku kwa lita = Jumla ya Ruzuku kwa mwezi (siku 30) Γ· Jumla ya matumizi ya mafuta ya petroli na dizeli kwa mwezi (siku 30)
= Tsh 100,000,000,000 Γ· lita 327,023,176.912
= Tsh 305.78 kwa lita

Bei ya mafuta baada ya ruzuku
= Bei ya kamili - Ruzuku kwa lita
= Bei kamili - Tsh 305.78

Hivyo:
Bei ya mafuta kwa lita baada ya ruzuku = Bei ya kamili - Tsh 305.78

Hivyo mafuta ya petroli na dizeli yatakua na punguzo la Tsh 305.78 baada ya kuwekwa ruzuku ya mwezi wa sita iliyotolewa.

Hili jedwali linaonyesha ruzuku kwa kila lita ya mafuta iliyowekwa na EWURA.

 
We- umefanya analysis?
 
Hivi Zanzibar ni mbali kiasi wameshindwa kwenda kuuliza kule wamewezaji kuuza mafuta kwa 2600/l pasipo na ruzuku?

Hapo si imetolewa ile 100/l tu iliyowekwa kienyeji,kuna ruzuku ipi tena hapo!
 

Ili mkokotoo wa bei mpya uwe na thamani ungetolewa mkokotoo wa bei iliyonunua mafuta ya lita 118,594,024 yaliyokuwa kwenye maghala April 1, 2022 dhidi ya mwelekeo wa bei za mafuta kwa kuanzia na lita 86,256,000 za dizeli kwenye meli zilizowasili hivi karibuni. Vingivevyo ruzuku ya billioni 100 (100B) itawanufaisha wauzaji tu, huku watumiaji na wananchi wakidanganywa kuwa Serikali ni sikivu na inajali.

Serikali ingekuwa sikivu, kwa suala la bei ya mafuta ingeweka utaratibu wa kuhakikisha lita 118,594,024 yaliyokuwa kwenye maghala April 1 yanauzwa kwa bei ya zamani kwanza. Hiyo ingewezekana kwa kuwa kila mwagizaji na mwuzaji anatunza hesabu ya mafuta aliyokuwa nayo na anayoagiza.

Tukubali au la ukweli ni kwamba ni kundi dogo la Wananchi ndilo linafaidika katika Serikali iliyoko madarakani
 
Faida ya kushusha bei ya mafuta ilikuwa na bei ya vitu vingine vishuke kuleta unafuu wa maisha.

Lakini sasa kama tunaambiwa kushusha bidhaa zingine inahitaji mchakato mrefu ,kwa kweli inasikitisha sana
 
Mbona kama punguzo ni 306 Tsh mkuu.
DSM mafuta ya petroli mwezi May yalikuwa yanauzwa Sh 3,148. Mwezi June bei itakuwa Sh 2,994. Sasa hilo punguzo la Sh 306 linatoka wapi? EWURA wanatudanganya kwamba mwezi May bei ya petrol DSM ilikuwa Sh 3,301 ili ku justify punguzo la Sh 306. Hakuna kituo chochote cha mafuta DSM kilichokuwa kinauza petroli kwa bei hiyo.

Hivyo kwa DSM punguzo halizidi Sh 154 kwa lita ya petroli na huku kwenye mikoa ya mbali halizidi Sh 107 kwa lita. Kwa hiyo Sh 100 billion haitakuwa na impact yo yote kwenye kudhibiti kuendelea na mfumuko wa bei.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…