Kukokotoa punguzo la bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwa mwezi wa sita 2022 baada ya kuongezewa ruzuku ya billioni 100 (100B)

Kukokotoa punguzo la bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwa mwezi wa sita 2022 baada ya kuongezewa ruzuku ya billioni 100 (100B)

DSM mafuta ya petroli mwezi May yalikuwa yanauzwa Sh 3,148. Mwezi June bei itakuwa Sh 2,994. Sasa hilo punguzo la Sh 306 linatoka wapi? EWURA wanatudanganya kwamba mwezi May bei ya petrol DSM ilikuwa Sh 3,301 ili ku justify punguzo la Sh 306. Hakuna kituo chochote cha mafuta DSM kilichokuwa kinauza petroli kwa bei hiyo.

Hivyo kwa DSM punguzo halizidi Sh 154 kwa lita ya petroli na huku kwenye mikoa ya mbali halizidi Sh 107 kwa lita. Kwa hiyo Sh 100 billion haitakuwa na impact yo yote kwenye kudhibiti kuendelea na mfumuko wa bei.
Mimi naona punguzo lipo sahihi kimahesabu. Kwasababu mimi kwa hesabu nilizofanya, kiukweli naona zipo sahihi.
 
Zinafichwa kwa sababu wanazozijua wao ili tuendelee kupigika. TRA ndiyo wanakusanya kodi za mafuta yanayoingia nchini bandarini kwa matumizi yetu na yale ya transit kila siku. Hawataki kuweka takwimu hizi public.

Na tutaendelea kutumia price peak ya March 2022 ya USD 139 per barrel of crude oil ambayo ilidumu kwa siku chache tu. Kuanzia April 2022 bei haijazidi USD 107 kwa pipa.

Haya bei mpya EWURA wameshatoa. Punguzo ni Sh 107 tu wakidai mafuta yanayokuja na yatakayokuja mwezi wa July yalinunuliwa mwezi March 2022. Ni bongoland.
Labda yawezekana kuna watu humu wanajua pengine, wanaweza kutusaidia. Au tungeandikia uzi kuuliza.
 
Back
Top Bottom