Kukomesha utekaji serikali ipige marufuku vikundi hivi vya kisiasa kama itaweza

Wasiojulikana waanza kujulikana na kuthihirisha watekaji na wauaji kwa sehemu kubwa ni vyombo vilivyoaminiwa na Wananchi kulinda mali na maisha yao. Hii ni dalili ya FAILED STATE
Vyombo hivi havijaaminiwa na wananchi, ni vya watawala dhidi ya watawaliwa.
 
Sababu SSH hana ushawishi atatumia zaidi Polisi usalama, Tamisemi / tume ya uchaguzi, rushwa, wasiojulikana, ubabe, watu kupotezwa, kutekwa na machawa ili kutawala na kushinda chaguzi zote mbeleni, pia kuwatuliza watu anaowaona tishio kwake.
 
Tumekua tukishuhudia utekaji wa watu nchini vikifanywa na eti wasiojulikana! Hawa wasiojulikana ni watanzania ambao huenda wamejiambatanisha na vyama vya siasa, hata hivyo ni CCM tu ndiyo ina vikundi vinavyojulikana kama Chawa, Uhamasishaji, Wadudu na Green Guard(Umoja wa vijana), hawa huenda wanaweza kuwa wanatumia kauli ya ukinizingua chawa wangu hawatakubali, na tukiangalia utekaji unawakumba mashabiki wa upinzani zaidi kuliko wa CCM.

Kutokana na nilivyoeleza ni vizuri Serikali ikapiga marufuku vikundi vyote hivi wakati huu tunaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa na wa Rais na Wabunge ambako kutazuka wimbi la vikundi vya ulinzi.
Itapigaje marufuku wakati serikali yenyewe ndio inaratibu huo utekaji.
 
Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute.​

Tumekua tukishuhudia utekaji wa watu nchini vikifanywa na eti wasiojulikana! Hawa wasiojulikana ni watanzania ambao huenda wamejiambatanisha na vyama vya siasa, hata hivyo ni CCM tu ndiyo ina vikundi vinavyojulikana kama Chawa, Uhamasishaji, Wadudu na Green Guard(Umoja wa vijana), hawa huenda wanaweza kuwa wanatumia kauli ya ukinizingua chawa wangu hawatakubali, na tukiangalia utekaji unawakumba mashabiki wa upinzani zaidi kuliko wa CCM.

Kutokana na nilivyoeleza ni vizuri Serikali ikapiga marufuku vikundi vyote hivi wakati huu tunaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa na wa Rais na Wabunge ambako kutazuka wimbi la vikundi vya ulinzi.

Kama ndio inawatuma? Ikate mkono wake wenyewe?
 
Back
Top Bottom