Kukopeshana hela mtaani kwa riba ni biashara iliyoshamiri na inalipa sana

Ukilangua gunia la mpunga shilingi 50,000 na ukaja kuliuza dar shilingi 80,000 hiyo ,hiyo faida ya elfu 30 sio Riba mkuu??

Sio riba mkuu hiyo ni faida kumbuka kuwa hapo umenunua na umekuja kuuza haijalishi umeuza kiasi gani hata ukiuza milioni sio riba.

Kwenye kuuza na kununua kuna makubaliano ya bei husika ya bidhaa, pia kuna kupunguziana bei kama discount yani vile mtakavyokubaliana na mteja.

Halaf pia, hapo kinachotoka ni bidhaa na inayoingia ni pesa ndugu wala sio vitu vinavyofanana ni vitu viwili tofauti kabisa.

Riba ni pale unapotoa kitu halaf baadae ukaja kurudisha au kulipa kwa zaidi ya ile bei au idadi uliyochukua mwanzo, aidha itategemea na pesa itakavyokuwa kwenye soko la dunia nikimaanisha labda wakati nakupa ilikuwa chini then uliponirudishia hela imepanda unaweza kurudisha kutokana na thamani itakavyokuwa wakati huo unarudisha, ila pia inatakiwa kuangalia wakati mnapeana thamani yake ilikuwaje ili mjue mtakaporudishiana itakuwaje.

Na pia, riba hasa ipo katika vitu au mali au bidhaa zinazofanana nikimaanisha nafaka kwa nafaka, dhahabu kwa dhahabu au fedha kwa fedha. Wala sio bidhaa kwa fedha, au nafaka kwa dhahabu laa.

Inaweza kuwa riba katika mfumo huo pindi tu itakapokuwa mwenye mali akasema bwana ee imekaa siku nyingi kwa hiyo kila baada ya siku kadhaa itaongezeka kiasi kadhaa coz umekaa siku nyingi hapo nayo hiyo itakuwa ni riba ndugu yangu. Kama utakuwa hujaelewa sehemu unaweza ukaniuliza tu nikakuelewesha wala usjali ndugu yangu.

Karibu Sana.
 
Kasome financial market vizuri, utaelewa nilichokimaanisha.



Asubuhi njema.
 

Mkuu. Ni financial/ lending institutions zenye kibali cha BOT pekee ndio zenye haki kisheria kukopesha na kuweka riba. Hapo kwenye mkataba kwakutumia ujanja hua nawashauri wateja wangu nikiwaandikia mkataba... kwa mfano mtu anakuja kumkopa mteja wangu laki moja na mteja wangu anataka faida ya elfu ishirini.. basi namuandikia mkataba ambao unasema mkopaji amekopwa laki na ishirini bila riba na anatakiwa kurudisha pesa hiyo baada ya mwezi ili hali amechukua laki moja. Ukiweka riba asipolipa mkaenda mahakamani , mkopeshaji imekula kwake kwani mkataba huo utakua hauna nguvu kisheria ( null and void from abi initial) .
 
Mimi kwangu riba kwa sh laki 1 ni sh 40,000 sio ghali.
 
Kasome financial market vizuri, utaelewa nilichokimaanisha.



Asubuhi njema.

Sisi hatufati maandiko ya mzungu na wala hatuongozwi na mzungu kama nyie tunafata maandiko ya ALLAH na tunaongozwa na kitabu chake.

Nawe pia.
 
Sisi hatufati maandiko ya mzungu na wala hatuongozwi na mzungu kama nyie tunafata maandiko ya ALLAH na tunaongozwa na kitabu chake.

Nawe pia.
Kweli mkuu, mwambie hamuongozwi na mzungu bali mnaongozwa na kitabu cha Mwarabu
 
Kitabu cha ALLAH sio cha mwarabu. Quran.
Kimeandikwa na nani?
Kinasambazwa na nani?

Kama hupendi kuudhiwa hasa huu mwezi mtukufu kwako usiingize kejeli za kidini za wengine utaharibu swaumu yako, vinginevyo labda hujafunga na unadhihaki Mola wako
 
Quran imeandikwa kwa lugha gani?
Hawezi kujibu, atakwambia kimeshushwa.
Swali je? Kinaendelea kushushwa au kinaandikwa?
Aliyeshushiwa ni mzungu?
Kilishushwa kimeandikwa kwenye karatasi, magome au nguo?
Kilitunzwa je? Na kilisambazwa je?
 
Kimeandikwa na nani?

Haya kama kingeandikwa na mswahili haiwezi kuwa mmiliki ni mswahili. Unajua akili tumepewa ili kuweza kutafakari jambo kabla ya kutenda, jaribu kugeuza shilingi upande wa pili utaona ilivyo tofauti.

Biblia imeandikwa na nani...?. Well, walioandika ndio wamiliki au ndio wenye nayo...?. Yale magazeti ya kila siku wale wanaoandika ndio wamiliki...?.

Kinasambazwa na nani?

Hili swali pia jibu lako unaweza kulipata hapo juu pia, je wasambazaji wanaweza kuwa ni wamiliki wa kitu wanachokisambaza kwani...?

Kama hupendi kuudhiwa hasa huu mwezi mtukufu kwako usiingize kejeli za kidini za wengine

Wapi nilipoingiza kejeli za kidini ndugu...?. Na ndio mana hapo juu nikasema akili tumepewa ili tuweze kufkiri jambo kabla ya kutenda. Akili yako ulishindwa kuifikirisha kwa sababu huyo jamaa alinitaka nikasome financial market kwa asilimia kubwa kabisa ni kitabu kilichoandikwa na mzungu ambapo siwezi kuongozwa nacho coz sisi kama waislam tunafata kitabu kitakatifu ambacho ni QURAN kina muongozo kwetu juu ya kila kitu ikiwemo na hiyo riba. Na ndio nikamwambia sifuati kitabu cha mzungu hiko cha financial market coz nna kitabu kinachoniongoza. Sasa wapi nilipoweka kejeli za kidini ndugu...?

utaharibu swaumu yako, vinginevyo labda hujafunga na unadhihaki Mola wako

Siwezi kuharibu swaumu yangu hata kidogo kwa jambo ambalo haliwezi kuharibu swaumu yangu hata kidogo. Nipo kwenye swaumu na wala haiwezi kuharibiwa kwa vitu visivyo na mashiko kama hivyo ndugu.

Karibu Sana.
 
Biashara ya kukopa kwa riba au kukopesha kwa riba ni dhambi kwa wote wawili, kuanzia kwa mkopaji na mkopeshaji. Lakini huo ni mtazamo kwa IMANI yangu!!!!!!
 
Shukrani sana mkuu kwa nyongeza ya elimu uliyonipa, kwahiyo sasa kwamfano na vile vikundi kwa VICOBA pia vinasimamia humu humu kwenye maelezo yako?
 
Hawezi kujibu, atakwambia kimeshushwa.
Swali je? Kinaendelea kushushwa au kinaandikwa?
Aliyeshushiwa ni mzungu?
Kilishushwa kimeandikwa kwenye karatasi, magome au nguo?
Kilitunzwa je? Na kilisambazwa je?

Nimeshajibu tayari.
 
Mkopeshe mtu halafu ahame mtaa usiku usiku ndio utajua vizuri faida na hasara ya hiyo kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…