Kukosa nguvu mwili mzima usiku nikiwa nimelala

Kukosa nguvu mwili mzima usiku nikiwa nimelala

MOODYGUY

Member
Joined
Jan 10, 2012
Posts
20
Reaction score
2
Habar zenu wanaJF, mi ninatatizo linanisumbua sana tokea zamani kama miaka minne iliyopita japo liliacha lakini sasa limeanza kurudi tena mala 1 moja, ni tatizo la kukosa nguvu mwili mzima usiku ukiwa umelala kiasi cha kushindwa kugeuka au hata kunyanyua kiungo chochote cha mwili japo unakua unajitambua, naomba msaaada wenu wakubwa.
 
Huwa wanaita kitu kama jinamizi kama niko sawa Kiongozi MziziMkavu tuchambulie.

Kwa upande wangu nafikiri ni ukiwa mtu wa kujishindilia kula na tabia ya kumaliza kupata chakula na kulala hapo hapo bila ya kuupa mwili mapumziko japo saa nzima kabla ya kulala.

Kingine ni namna ya ulalaji inachangia pia hasa pale unapokuwa umefakamia chakula
 
Habar zenu wanaJF, mi ninatatizo linanisumbua sana tokea zamani kama miaka minne iliyopita japo liliacha lakini sasa limeanza kurudi tena mala 1 moja, ni tatizo la kukosa nguvu mwili mzima usiku ukiwa umelala kiasi cha kushindwa kugeuka au hata kunyanyua kiungo chochote cha mwili japo unakua unajitambua, naomba msaaada wenu wakubwa.
Pole sana jitahidi kuwa ukisha maliza kula chakula cha usiku ukae kwa muda wa masaa 2 bila ya kulala baada ya hapo lala na ukilala usilale kichalichali yaani

usilale wakati uso wako umeuelekeza juu mbinguni ulale ubavu wa kulia kwa muda wa saa nzima kisha geuka upande wa kushoto ulale tena ubavu wa kushoto uwe unalala hivyo Kiislam

slam ndivyo wanavyo lala usijali mambo ya dini ukiwa wewe ni mkristo wakati wa kulala omba dua kisha ulaleikiwa wewe ni muislam toa shahada kisha soma Sura za Quran kisha mtaje Jina

la Mwenyeezi Mungu Ya-Allah kwa wingi mpaka utakapopata usingizi. Hilo ni jinamizi Shetani mbaya anakubana mwili wako usingizini unakosa nguvu mwilini mwako. Ki-Sayansi hawaamini Majinamizi.


553432_425604320825811_1687825358_n.jpg


NJIA ZA HARAKA ZA KUEPUKANA NA KUKABWA NA JINAMIZI

1.Ikikutokea hali hiyo jaribu kuvuta pumzi nyingi ndani kwa sababu pumzi peke yake ndio unayoweza kuidhibiti ukiwa umekabwa.

2.Jiepushe kulala chali.

3.Punguza mawazo mengi.

4.Lala katika muda mzuri na jaribu kupata muda mrefu wa usingizi masaa 8 mpaka 10.

5.Jaribu kuwa na muda maalum wa kulala ikiwa ni saa 3 basi iwe muda huo wakati wote.

6.Jaribu kula vizuri kabla hujalala.

7.Kumbuka kwamba pamoja ya kuwa hali hii inatisha lakini haina hatari yoyote.

8.Ukihisi unakabwa jaribu sana kujitingisha, hali ya kukabwa itakwisha.

9.Ukiona kama unataka kukabwa amka kaa chini kwa dakika 5 halafu lala tena.
 
Back
Top Bottom